Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Zingatia mambo haya wakati wa kunyonyesha Mtoto

Zingatia mambo haya wakati wa kunyonyesha Mtoto

KANUNI ZA UNYONYESHAJI BORA

(1) Mnyonyeshe mtoto maziwa ya mama peke yake kwa Kipindi cha Miezi sita bila kuchanganyiwa na kitu chochote yaani kwa kitaalam tunaita “EXCLUSIVE BREASTFEEDING”

(2) Baada ya Miezi sita ya Mwanzoni,anza kidgo kidogo kumchanganyia mtoto maziwa ya mama na vyakula vingine,na usiache kumnyonyesha mpaka atakapofikisha umri wa miaka 2 au 3.

(3) Maziwa ya mama yanakata kiu ya mtoto kwahyo usimpe mtoto na maji, kumbuka maziwa ya mama yamegawanyika katika sehemu kuu tatu,

(i) maziwa ya kwanza hutoka kama maji na ndyo hukata kiu ya mtoto

(ii)maziwa ya kati ni mepesi

(iii)na maziwa ya mwisho ni mazito na ndyo humshibisha mtoto vizuri.

Kwahyo ili mtoto ashibe lazima mama amnyonyeshe mtoto vizuri na kwa mda wa kutosha,mpka mtoto akute yale maziwa ya mwisho mazito,bila hivo mtoto hatashiba

(4) Fanya usafi wa maziwa au matiti yako kabla ya kuanza kumnyonyesha mtoto

(5) Mnyonyeshe mtoto kila mara anapohitaji kunyonya yeye,sio kila unapohitaji wewe

(A) FAIDA ZA UNYONYESHAJI BORA KWA MTOTO

1️⃣ Mtoto kupata virutubisho Vyote

Maziwa ya mama humpatia mtoto virutubisho vyote anavyohitaji katika miezi 6 ya mwanzo toka kuzaliwa. Hivyo kufanya maziwa ya mama kuwa lishe muafaka kwa mtoto. Yana uwiano mzuri wa wanga, protini, mafuta, vitamini pamoja na madini. Vilevile maziwa haya yanameng’enyeka vyema kuliko maziwa ya kopo.

2️⃣ Kinga Dhidi ya Magonjwa

Maziwa ya mama hupunguza hatari ya mwanao kupata asthma au mzio. Pia yana kingamwili (antibodies) wanaopambana na virusi pamoja na bakteria wanaosababisha magonjwa.

Tafiti zimeonesha kwamba watoto wanaotunzwa kwa maziwa ya mama bila ya lishe nyingine mpaka miezi sita wanaepuka hatari za kupata maambukizi ya ugonjwa wa masikio na magonjwa ya njia ya upumuaji. Maziwa pia yameonekana kusaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa kama kisukari na uzito kupindukia.

3️⃣ Kuimarisha ubongo wa Mtoto ikiwemo uwezo wa Kufikiri

Ifahamike kuwa kwamba maziwa ya mama huchangia kuongeza werevu kwa watoto (IQ).

4️⃣ Kuimarisha mahusiano ya Mama na Mtoto yaani BONDING

Tena maziwa ya mama na kitendo cha kunyonyesha huchangia kutengeneza muunganiko katika mahusiano ya mtoto na mama ambayo hutokana na kule kugusana kati ya mama pamoja na kutazamana wakati wa kunyonyesha na hali hii pia huwafanya watoto kujihisi salama wanapokuwa na mama zao.

5️⃣ Kupunguza vifo vya Gafla kwa watoto

Mwisho na muhimu, je wajua kwamba maziwa ya mama husaidia kumpunguzia mwanao hatari ya kupata kifo cha ghafla (sudden infant death syndrome)?

(B) FAIDA ZA UNYONYESHAJI KWA MAMA

Je, kuna faida zozote za unyonyeshaji kwa mama?

(1) Unyonyeshaji husaidia kutoa kichocheo cha oxytocin ambacho husababisha mji wa uzazi wa mama (uterus) kurudi katika umbo na hali yake ya kawaida kabla ya kupata ujauzito na huweza pia kusaidia kupunguza kutoka damu ukeni baada ya kujifungua.

(2) Unyonyeshaji pia huchangia kuchoma kalories ili kumsaidia mama kupunguza uzito alioupata wakati wa ujauzito ili arudi katika umbo lake la awali mapema iwezekanavyo.

(3) Unyonyeshaji husaidia kushusha hatari ya kupata saratani ya matiti na hata saratani ya mfuko wa mayai (ovarian cancer). Vilevile unyonyeshaji husaidia katika kupunguza hatari ya kupata osteoporoisis.

(4) Mwisho kabisa unyonyeshaji husaidia kupunguza matumizi ya pesa kwani huna haja ya kununua maziwa ya kopo, nk. kwani mama maziwa yake tayari yapo kwa usafi unaotakiwa.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.