Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Dalili za mtu anaetaka kujiua ni pamoja na

Tarehe 10 Septemba ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kuzuia Kujiua Duniani. Lengo la siku hii ni kuikumbusha jamii, familia na mtu mmoja mmoja umuhimu wa kuwa sehemu ya kuokoa maisha ya watu wenye dalili za kuelekea kujiua.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonesha kuwa takribani watu milioni 4 huwaza au kujaribu kujiua duniani, ambapo miongoni mwao, laki 8 huchukua uamuzi wa kujiua.

Vitendo hivi huathiri watoto, wazazi, wenza, familia, marafiki na jamii kwa ujumla.

Dalili za mtu anaetaka kujiua ni pamoja na:

– kujitenga na watu wengine au shughuli za kijamii

– kuzungumza au kutishia kujiua

– kuonekana mwenye huzuni na kuonesha dalili za kukata tamaa kwa kiasi kikubwa na kutokuwa na tumaini

– kujiona mwenye hatia au mkosaji na kujichukia au kujilaumu mwenyewe na kujiona hafai kuishi tena

– dalili za sonona au msongo wa mawazo

– kugawa vitu anavyomiliki bila sababu ya msingi

– kuaga familia na marafiki kana kwamba hawataonana tena

– kuandaa njia za kutaka kujiua mfano kukusanya na kuhifadhi dawa nyingi wakati siyo mgonjwa

– kufanya mambo yanayoweza kumdhuru mfano kuendesha gari kizemve

Ukiona mtu ana dalili za kujiua, toa taarifa haraka iwezekanavyo kwa kuongea nae ili kumtia moyo na kisha msaidie afike kituo cha huduma za afya kwa huduma zaidi.

Aidha, ikiwa mtu huyo ameongea nawe kuhusu kujiua usimuache peke yake; omba msaada haraka kutoka kwa wanafamilia au marafiki.
#elimu_ya_afya

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.