Tatizo la Kukojoa Mara kwa Mara,chanzo chake na Tiba
Tatizo la Kukojoa Mara kwa Mara,chanzo chake na Tiba
Kukojoa mara kwa mara baada ya kupata kinywaji, Unaweza kupatwa na hali ya kukojoa mara kwa mara baada ya kunywa vinywaji vingi kama vile Maji mengi, vinywaji vyenye Caffeine,Pombe n.k
Hali ambayo wakati mwingine inaweza kuleta usumbufu hasa wakati ukiwa Umelala Usiku,
Lakini pia Kukojoa Mara kwa Mara inaweza kuwa kiashiria cha kukuonyesha kwamba kuna kitu hakipo Sawa,
Haya hapa ni baadhi ya Matatizo ambayo kiashiria chake Mojawapo ni Mtu kukojoa Mara Kwa Mara;
1. Mtu kuwa na matatizo kwenye Kibofu cha Mkojo
2. Mtu kuwa na matatizo kwenye Figo,Ureter n.k
3. Mtu kuwa na tatizo la KISUKARI
4. Mtu kuwa na matatizo kwenye tezi dume yaani prostate gland problems
5. Mtu kuwa na maambukizi kwenye njia ya mkojo yaani urinary tract infection-UTI
6. Mtu kuwa na tatizo la kuvimba kwa Urethra yaani urethritis
7. Mtu kuwa na Uvimbe kwenye eneo la Pelvic, Uvimbe kwenye kibofu cha Mkojo n.k
8. Hali ya Kuwa Mjamzito, wakina mama wengi wajawazito hupatwa na hali ya kukojoa mara kwa mara,
Hii ni kutokana na Presha au mgandamizo wa mtoto anayekuwa tumboni dhidi ya kibofu cha Mkojo, hali ambayo hupelekea eneo(room) kwenye kibofu cha Mkojo kupungua,
9. Mtu Kupatwa na tatizo la kuvimba kwa kuta za kibofu yaani kwa kitaalam hujulikana kama interstitial cystitis
10. Mtu kupatwa na tatizo la Mawe kwenye Njia ya Mkojo(urinary tract stones)
11. Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile dawa jamii ya diuretics
12. Huduma ya radiotherapy
13. Kushambuliwa na magonjwa mbali mbali ya Zinaa(sexually transmitted infections (STIs)
14. Mtu kuwa na matatizo ya Neva yaani neurological problems n.k
MATIBABU YAKE NI YAPI?
Matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake,kama nilivyokwisha kueleza hapo Juu.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.