Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

UGONJWA WA EBOLA,DALILI NA MATIBABU YAKE

UGONJWA WA EBOLA,DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA,HISTORIA YAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Ugonjwa wa Ebola yaani Ebola virus Disease(EVD) ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambao hujulikana kama Ebola virus,

Virusi hawa wapo wa aina mbali mbali kama vile Ebola-Sudan Strain n.k

HISTORIA YA EBOLA

Kwa mara ya kwanza Ugonjwa wa Ebola ulihusishwa kutokea huko ZAIRE(CONGO) mwaka 1976. Ambapo aina tano za Virusi vinavyosababisha Ugonjwa wa Ebola vilikuja kugundulika hapo baadae,baada ya maeneo mengi kuathiriwa na Ugonjwa huu.

Njia Ambazo Ugonjwa Wa Ebola Huambukizwa

Ugonjwa huu  huweza kusambazwa kwa njia mbali mbali kama;

– Kupitia kugusana na mgonjwa wa Ebola

– Kupitia kwenye Vidonda vilivyopo wazi(open wound)

– Kupitia kugusana na mgonjwa au mnyama aliyekufa mwenye Virusi hawa wa Ebola

– Kupitia kushika au kugusa matapishi ya mgonjwa wa Ebola

– Kupitia maji maji ya mwili wa Mgonjwa,mate,jasho au Damu yake

– Kupitia kugusa au kushika kinyesi au Mkojo wa mgonjwa wa Ebola

– Lakini pia Mtu huweza kupata Ugonjwa wa Ebola kwa Kupitia Wanyama pia

– Kushiriki tendo la Ndoa na Mgonjwa wa Ebola

– Kushirikiana Vyombo vya Kula pamoja na chakula na Mgonjwa wa Ebola

– Kushika mashuka au nguo za mgonjwa wa Ebola bila kuvaa kinga kama Gloves mikononi n.k

 

Hakuna dalili za Moja kwa moja za Ugonjwa wa Ebola, Japo mgonjwa ataonyesha dalili kama za magonjwa mengine kwani mwili ukipata shida yoyote lazima uonyeshe matokeo, Na dalili hizo ni pamoja na;

  1. Kupatwa na shida ya kukauka kwa koo
  2. Mgonjwa kupata homa kali pamoja na mwili kuchoka sana
  3. Maumivu makali ya kichwa
  4. Maumivu kwenye joint,misuli pamoja na viungo mbalimbali vya mwili
  5. Ngozi ya mwili kuwasha
  6. Kusikia kichefu chefu pamoja na kutapika
  7. Kupatwa na tatizo la kuharisha
  8. Kupata matatizo ya kwenye Ini
  9. Kupata matatizo ya Figo
  10. Kutokwa na Damu sehemu zote zenye matundu mwilini,kama kwenye masikio,pua na macho.
  11. Hamu ya chakula kupotea
  12. Kupata shida wakati wa upumuaji
  13. Kupata maumivu makali ya kifua
  14. Kubadilika rangi ya macho na kuwa Nyekundu
  15. Kupatwa na Homa kali, degedege
  16. Kutapika matapishi yenye damu
  17. Kuharisha na kutoa damu machoni
  18. Kutokwa na damu katika matundu ya mwilini kama vile; Puani,Njia ya haja kubwa,njia ya haja ndogo,mdomoni,masikioni,machoni n.k Hali ambayo hupelekea kifo cha Muda mfupi

VIPIMO VYA EBOLA

Mgonjwa wa Ebola hufanyiwa vipimo maalum ambavyo huhusisha sampuli za Damu,Mate,jasho N.k kutoka kwa Mgonjwa, Japo mara nyingi vipimo hivo hufanyika baada ya mtu kuhisi ugonjwa huu au kuonyesha baadhi ya Dalili za Ugonjwa huu wa Ebola.

MATIBABU YA UGONJWA WA EBOLA.

Mpaka sasa hakuna matibabu au Dawa ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Ebola. Bali watu hutibu dalili za Ugonjwa kama ilivyo kwa magonjwa mengi yanayosababishwa na Virusi kama CORONA.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.