Hizi hapa ni Baadhi ya dalili za ugonjwa wa UKIMWI
Hizi hapa ni Baadhi ya dalili za ugonjwa wa UKIMWI
DALILI ZA UKIMWI
Kwa asilimia kubwa baada ya maambukizi ya virusi vya ukimwi au HIV/AIDS,
Huchukua muda wa wiki 2 mpaka 4 kwa dalili kuanza kuonekana kwa mtu.
DALILI HIZO ZA UKIMWI(HIV/AIDS) NI PAMOJA NA;
1. Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na homa za mara kwa mara
2. Kupatwa na shida ya mafua ambayo hayaishi
3. Kupatwa na shida ya maumivu makali ya kichwa mara kwa mara
4. Kupatwa na maumivu ya misuli pamoja na joints
5. Mwili kuchoka sana kuliko kawaida
6. Mwili kuanza kuwa na rashes
7. Kutokewa na vidonda mdomoni,kooni,kupata maumivu wakati wa kumeza kitu,
8.Tezi za Lymph au lymph node kuanza kuvimba hasa eneo la shingoni n.k
9. Mtu kupatwa na tatizo la kuharisha
10. Mtu kutoa sana jasho kuliko kawaida
11. Uzito wa mwili kupungua kwa kasi zaidi(body weight loss)
12. Mtu kuanza kupatwa na kikohozi cha mara kwa mara n.k