Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Jinsi Ukimwi kuambukizwa,Soma zaidi hapa jinsi ugonjwa wa ukimwi huambukizwa

Jinsi Ukimwi kuambukizwa,Soma zaidi hapa jinsi ugonjwa wa ukimwi huambukizwa

JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA UKIMWI

Baadhi ya njia hizi hapa chini zitakusaidia kujikinga na Maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi, Soma hapa..!!!

– Epuka kushare vitu vyenye ncha kali kama vile nyembe,sindano,Pin n.k

– Epuka kushare mswaki na mtu yoyote

– Epuka tabia ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile(Anal Sex),

Tafiti zinaonyesha njia hii ya kufanya mapenzi Kinyume na maumbile yaani Anal Sex huongeza uwezekano wa mtu kupata maambukizi ya UKIMWI kwa asilimia kubwa sana

– Epuka ngono zembe, tumia kinga(Condom),

Matumizi sahihi ya Condom huweza kukusaidia kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kwa asilimia kubwa

– Epuka tabia ya kuwa na wapenzi wengi(Multiple Sexual partners),

Tabia hii huongeza hatari ya mtu kupata maambukizi ya ukimwi kwa kiwango kikubwa sana

– Tibu magonjwa yote ya Zinaa yaani Sexual Transmitted diseases(STD’s) kama chlamydia,kaswende,kisonono n.k

magonjwa ya Zinaa huongeza uwezekano wa mtu kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi,hivo hakikisha unapata tiba.

– Fanya vipimo mara kwa mara, na endapo umekuwa kwenye hatari yoyote ya kupata maambukizi kama vile;

• kuchomwa na sindano wakati wa kumhudumia mgonjwa wa ukimwi

• kubakwa

• Kushiriki tendo la ndoa na muathirika wa virusi vya ukimwi n.k

Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya ili wakupatie dawa za kukukinga usipate maambukizi yaani Post-exposure prophylaxis(PEP).

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.