Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la Gallstones,dalili na Tiba yake

Tatizo la Gallstones,dalili na Tiba yake

Gallstones ni tatizo ambalo huhusisha amana ngumu(hardened deposits) ya maji ya usagaji chakula ambayo yanaweza kuundwa kwenye kibofu chako cha nyongo yaani gallbladder.

DALILI ZA TATIZO HILI LA GALLSTONES

Tatizo hili linaweza lisionyeshe dalili zozote ila Endapo gallstones zimeziba kwenye mrija huweza kusababisha dalili kama hizi;

– Maumivu ya gafla na ambayo yanaongezeka sehemu ya juu kulia mwa tumbo

– Maumivu ya gafla na ambayo yanaongezeka katikati ya tumbo, chini ya mfupa wa matiti(breastbone) n.k

– Maumivu ya mgongo, maumivu kwenye bega lako ka kulia

– Kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika

– Ngozi ya mwili kuanza kubadilika rangi na kuwa manjano(jaundice)

– Kupata homa kali na mwili kutetemeka n.k

CHANZO CHA TATIZO HILI LA GALLSTONES

Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo inajulikana kusababisha gallstones kutengenezwa kwenye kibofu cha Nyongo, ila sababu hizi hapa chini huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili;

1. Nyongo kuwa na kiwango kikubwa sana cha cholesterol ndani yake

2. Nyongo kuwa na kiwango kikubwa sana cha bilirubin ndani yake

3. Tatizo la kifuko cha nyongo(gallbladder) kutokufanya kazi ya kutoa vitu(emptying) kwa usahihi

4. Jinsia ya Kike,Wanawake wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo hili kuliko wanaume

5. Kuwa na umri kuanzia miaka 40 au zaidi

6. Kuwa na shida ya Uzito mkubwa sana(Overweight/Obesity)

7. Kuwa Mjamzito

8. Kula vyakula vyenye kiwango kikubwa sana cha Mafuta

9. Kula vyakula vyenye kiwango kikubwa sana cha Cholestrol

10. Kula vyakula vyenye kiwango kidogo sana cha Nyuzi nyuzi(fibers)

11. Kuwa na tatizo la Kisukari(diabetes)

12. Kuwa kwenye Familia ambapo kuna mtu mwenye tatizo hili au amewahi kuwa na tatizo hili la Gallstones

13. Kuwa na matatizo mbali mbali ambayo huhusisha damu kama vile; sickle cell anemia, leukemia n.k

14. Kuwa na shida ya kupungua Uzito kwa Kasi Sana

15. Kutumia Dawa zenye kichocheo cha Estrogen kama vile vidonge vya uzazi wa mpango(oral contraceptives)

16. Kuwa na magonjwa mbali mbali ya Ini n.k

JINSI YA KUJIKINGA AU KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA TATIZO HILI LA GALLSTONES

– Epuka tabia ya kushinda na Njaa Mara kwa mara

– Kam una shida ya UZITO MKUBWA Punguza Uzito taratibu, Kutumia njia za kupunguza uzito kwa haraka sana huweza kuongeza hatari ya kupata tatizo hili

– Hakikisha unakula vyakula vyenye nyuzi nyuzi(fibers) za kutosha,punguza vyakula vya mafuta mengi pamoja na cholestrol nyingi

– Fanya mazoezi mbali mbali ya mwili n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.