Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Vitamin B1 faida kwa Watu wenye tatizo la maumivu makali ya Kichwa,kipandauso(Migraine)

Vitamin B1 faida kwa Watu wenye tatizo la maumivu makali ya Kichwa,kpandauso(Migraine),

Baadhi ya watu husumbuliwa Sana na tatizo hili la maumivu makali ya kichwa ambalo kwa Kitaalam hujulikana kama kipandauso au Migraine,

Baadhi ya tafiti za hivi karibuni zimeonyesha kula mlo wenye virutubisho vingi vya Vitamin B hasa B1 au thiamine husaidia kupunguza hatari ya tatizo la kipandauso(Migraine).

Maumivu makali ya kichwa(migraine) wakati mwingine huweza kuzidi sana na kuwa vigumu kuyadhibiti,

Utafiti mpya ambao umechapishwa kwenye”Headache: The Journal of Head and Face Pain” umeonyesha kwamba,kula mlo wenye Vitamin B(thiamine) huweza kusaidia kuzuia tatizo la maumivu makali ya kichwa yaani  kipandauso au migraine kwa baadhi ya watu.

Utafiti huu umeonyesha uwepo wa protective factor ambazo husaidia kuleta matokeo mazuri kwa watu wenye shida hii ya kipandauso/ MIGRAINE.

Matokeo ya Migraine huweza kuhusisha maumivu makali ya kichwa ambayo hutokea upande mmoja,

Na maumivu haya huweza kuwa makali sana na wakati mwingine huambatana na dalili zingine kama vile;

Mtu kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika,

Msongo wa mawazo au Stress,mabadiliko ya vichocheo mwilini(hormonal changes) vyote hivi huweza kuhusika la tatizo la kipandauso au Migraine.

SOMA ZAIDI hapa tatizo hili la KipandaUso,Chanzo,Dalili na Tiba yake

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.