Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Watu ambao hulala chini ya Masaa 6 kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya Moyo na Kansa

Watu ambao hulala chini ya Masaa 6 kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya Moyo na Kansa,

Baadhi ya tafiti zimeonyesha watu wenye umri wa kati pamoja na Umri Mkubwa ambao hulala kuanzia masaa matano(5) kushuka chini wapo kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa mbali mbali ikiwemo magonjwa ya MOYO pamoja na Saratani/Kansa.

Moja ya UTAFITI huo ulifanyika kwenye chuo cha “University College London nchini Wingereza(UK) pamoja na Université Paris Cité, nchini Ufaransa(France),

ambapo ulionyesha, watu wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea ambao hulala kuanzia masaa matano(5) tu au chini ya hapo walikuwa kwenye hatari ya asilimia 30% kupata magonjwa mengi ya kudumu(chronic diseases) kuliko wale ambao angalau hulala kwa Masaa 7.

Na walipochukuliwa washiriki wenye umri wa miaka 70 hatari iliongezeka hadi asilimia 40%,

Na haya hapa ni baadhi ya magonjwa ambayo yalionekana kuweza kuwapata Zaidi watu kama hawa;

– Ugonjwa wa Kisukari(diabetes)

– Tatizo la Saratani au KANSA

– Magonjwa ya Moyo ikiwemo;

• Coronary heart disease

• Moyo kushindwa kufanya kazi(heart failure)

– Tatizo la kiharusi au STROKE

– Tatizo la chronic obstructive pulmonary disease(COPD)

– Ugonjwa wa Figo(Chronic kidney disease)

– Ugonjwa wa Ini(Liver disease)

– Tatizo la Depression

– Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu au Dementia

– Tatizo la Parkinson’s disease

– Tatizo la arthritis N.k

Pamoja na mambo mengi tunayofanya, lazima tujitahidi kupata muda wa kutosha wa Kulala, Usingizi ni muhimu pia kwa afya Zetu,

Ili kazi mbali mbali za MWILI zifanyike vizuri ikiwemo urekebishaji wa maswala ya Metabolism, endocrine system,Inflammatory regulation n.k lazima tupate muda wa kulala.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.