Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Jamii ikipata Elimu ya Kutosha dhidi ya Magonjwa kama EBOLA,inakuwa rahisi hata kuyadhibiti

Jamii ikipata Elimu ya Kutosha dhidi ya Magonjwa kama EBOLA,inakuwa rahisi hata kuyadhibiti

Magonjwa kama haya huanzia kwenye Jamii, na Wasambazaji wa kubwa ni Jamii, na Waathirika wakubwa ni hyo hyo Jamii, Hivo jamii lazima ihusishwe kwa asilimia 100% kwenye kupambana na magonjwa kama haya.

Jamii ikipata Elimu ya kutosha kwa Magonjwa kama Ebola, inakuwa rahisi sana kuweza kuyadhiti hata yakitokea.

Ni muhimu sana Kwa JAMII kujua magonjwa haya yapoje,Dalili zake, jinsi yanavyosambazwa na Jinsi ya Kujikinga.

SOMA ZAIDI HAPA DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA

Dalili za Ugonjwa Wa Ebola,Soma Hapa…

dalili hizo ni pamoja na;

  1. Mgonjwa kupata homa kali pamoja na mwili kuchoka sana
  2. Maumivu makali ya kichwa
  3. Maumivu kwenye joint,misuli pamoja na viungo mbalimbali vya mwili
  4. Ngozi ya mwili kuwasha
  5. Kusikia kichefu chefu pamoja na kutapika
  6. Kupatwa na tatizo la kuharisha
  7. Kupata matatizo ya kwenye Ini
  8. Kupata matatizo ya Figo
  9. Kutokwa na Damu sehemu zote zenye matundu mwilini,kama kwenye masikio,pua na macho.
  10. Hamu ya chakula kupotea
  11. Kupata shida wakati wa upumuaji
  12. Kupata maumivu makali ya kifua
  13. Kubadilika rangi ya macho na kuwa Nyekundu
  14. Kupatwa na Homa kali, degedege
  15. Kutapika matapishi yenye damu
  16. Kuharisha na kutoa damu machoni
  17. Kutokwa na damu katika matundu ya mwilini kama vile; Puani,Njia ya haja kubwa,njia ya haja ndogo,mdomoni,masikioni,machoni n.k Hali ambayo hupelekea kifo cha Muda mfupi

UGONJWA WA EBOLA,DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA,HISTORIA YAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Ugonjwa wa Ebola yaani Ebola virus Disease(EVD) ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambao hujulikana kama Ebola virus,

Virusi hawa wapo wa aina mbali mbali kama vile Ebola-Sudan Strain n.k

NJIA AMBAZO UGONJWA WA EBOLA HUAMBUKIZWA

Ugonjwa huu  huweza kusambazwa kwa njia mbali mbali kama;

– Kupitia kugusana na mgonjwa wa Ebola

– Kupitia kwenye Vidonda vilivyopo wazi(open wound)

– Kupitia kugusana na mgonjwa au mnyama aliyekufa mwenye Virusi hawa wa Ebola

– Kupitia kushika au kugusa matapishi ya mgonjwa wa Ebola

– Kupitia maji maji ya mwili wa Mgonjwa,mate,jasho au Damu yake

– Kupitia kugusa au kushika kinyesi au Mkojo wa mgonjwa wa Ebola

– Lakini pia Mtu huweza kupata Ugonjwa wa Ebola kwa Kupitia Wanyama pia

– Kushiriki tendo la Ndoa na Mgonjwa wa Ebola

– Kushirikiana Vyombo vya Kula pamoja na chakula na Mgonjwa wa Ebola

– Kushika mashuka au nguo za mgonjwa wa Ebola bila kuvaa kinga kama Gloves mikononi n.k

Vipimo Vya Ebola

Mgonjwa wa Ebola hufanyiwa vipimo maalum ambavyo huhusisha sampuli za Damu,Mate,jasho N.k kutoka kwa Mgonjwa, Japo mara nyingi vipimo hivo hufanyika baada ya mtu kuhisi ugonjwa huu au kuonyesha baadhi ya Dalili za Ugonjwa huu wa Ebola.

MATIBABU YA UGONJWA WA EBOLA.

Mpaka sasa hakuna matibabu au Dawa ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Ebola. Bali watu hutibu dalili za Ugonjwa kama ilivyo kwa magonjwa mengi yanayosababishwa na Virusi kama CORONA.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.