Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kila mwaka, inakadiriwa watoto milioni 15 huzaliwa kabla ya wakati(Watoto njiti au Premature),Na Zaidi ya watoto million 20 Wana Uzito Mdogo

Kila mwaka, inakadiriwa watoto milioni 15 huzaliwa kabla ya wakati(Watoto njiti au Premature),Na Zaidi ya watoto million 20 Wana Uzito Mdogo

Shirika la Afya Duniani-WHO linashauri zaidi huduma ya ngozi kwa ngozi yaani Kangaroo Care kwa ajili ya maisha ya watoto hawa wenye Uzito mdogo na ambao wamezaliwa kabla ya wakati.

WHO leo imezindua miongozo mipya ili kuboresha maisha na matokeo ya afya kwa watoto wanaozaliwa mapema (kabla ya wiki 37 za ujauzito) au wenye Uzito mdogo (chini ya kilo 2.5 wakati wa kuzaliwa).

Mwongozo huo unashauri kwamba huduma ya kugusa ngozi hadi ngozi na mlezi/Mzazi/Mama – yaani kangaroo care inapaswa kuanza mara tu baada ya mtoto huyu kuzaliwa, bila hata kupelekwa kwenye incubator kwanza.

Hili linaashiria mabadiliko makubwa kutoka kwa mwongozo wa awali, ambapo hapa walezi/wazazi/mama na watoto njiti wanaweza kukaa karibu, bila kutenganishwa, baada ya kuzaliwa.

Mwongozo huo pia hutoa mapendekezo ya kuhakikisha usaidizi wa kihisia, kifedha na mahali pa kazi kwa familia za watoto wadogo sana na wanaozaliwa kabla ya wakati, ambao wanaweza kukabiliwa na matatizo kwa sababu ya mahitaji ya utunzaji mkubwa na wasiwasi kuhusu afya ya watoto wao.

“Watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao wanaweza kuishi, kusitawi na kubadilisha ulimwengu – lakini kila mtoto lazima apewe nafasi hiyo,” alisema Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO. ”

Prematurity ni suala la dharura la afya ya umma. Kila mwaka, inakadiriwa watoto milioni 15 huzaliwa kabla ya wakati, ikiwa ni zaidi ya 1 kati ya 10 ya watoto wote wanaozaliwa duniani, na idadi kubwa zaidi – zaidi ya watoto milioni 20 – wana tatizo la uzito mdogo.

Idadi hii inaongezeka, na watoto hawa ndio chanzo kikuu cha vifo vya watoto chini ya umri wa miaka 5.

Kwa nchi zilizoendea watoto ambao wamezaliwa wiki ya 28 au zaidi na kabla ya kufika wiki 37 yaani kwa jina lingine watoto Njiti au Premature uwezekano wa Kuishi ni mkubwa ukulinganisha na nchi Maskini

Huduma ya Kangaroo Care,Kuzuia au kudhibiti maambukizi yoyote ya Magonjwa kwa watoto hawa pamoja na Unyonyeshaji wa maziwa ya Mama Pekee ni Muhimu sana kwa ajili ya Maisha ya Watoto hawa.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.