Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Lini Mwili Unarudi Kwenye Hali yake ya Kawaida Baada ya Kujifungua?

Lini Mwili Unarudi Kwenye Hali yake ya Kawaida Baada ya Kujifungua?

Kipindi tunachozungumzia hapa huanza tu baada ya mama kujifungua akiwa bado chumba cha kujifungua,

Na kipindi hiki huenda mpaka siku 42(week 6-8), kwa kitaalam hujulikana kama Postpartum.

Hivo basi toka siku Unajifungua,Mwili wako huanza mchakato wa kupona na kurudi kwenye hali yake ya kawaida,

Ambapo kwa makadirio huweza kuchukua week 6 mpaka 8, Mwili kurudi kwenye hali yake ya Awali.

Kama Umejifungua Hospitalini,Kwa hosptal nyingi,Mama baada ya kujifungua atawekwa Masaa 24 mpaka 48 kulingana na hali yake, huku wataalam wa afya wakiendelea kuangalia hali ya mama huyo.

Mama ataendelea kuangaliwa vitu muhimu kama vital Signs zote(ikiwemo joto la mwili,presha yake mapigo ya moyo n.k) bila kusahau kuangalia hali ya Kuvuja Damu,

Hii ni muhimu sana mama kuchunguzwa kama anaendelea kuvuja damu baada ya kujifungua,

Kwani baadhi ya wakina mama baada ya kujifungua huweza kupatwa na tatizo la kuvuja damu kupita kiasi baada ya kujifungua, tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Postpartum hemorrhage maarufu kama PPH,

Tatizo hili husababisha vifo kwa wakina mama wengi baada ya Kujifungua.

Mama baada ya kujifungua huweza kuendelea kupata vimaumivu kidogo,au tumbo kukaza yaani contractions/cramping au afterpains,

Watu wengi hufikiri Mama akishajifungua basi imeisha, Lakini ukweli ni kwamba, mwili huendelea na process mbali mbali kama hii ya tumbo kukaza ili kuzuia damu kuvuja zaidi kutoka kwenye Uterus.

Kwa hizi siku za mwanzoni,Mama baada ya kujifungua ataendelea kuona Damu damu,na uchafu mwingine,ambapo kadri siku zinavyokwenda hubadilika,hii hujulikana kwa kitaalam kama Lochia.

KUMBUKA: Damu damu tunayozungumzia hapa sio damu nyingi kama hii ya Mama ambaye amepatwa na tatizo la PPH,ambalo huweza kuondoa maisha yake.

Pia unaweza kuhisi vimaumivu ukeni mpaka utakapopona, na hasa kama ulichanika(tear) wakati wa Kujifungua.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.