Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dhana Potofu Kuhusu Ugonjwa wa Malaria na Maelekezo sahihi kuhusu dhana hizi, Soma zaidi hapa

Dhana Potofu Kuhusu Ugonjwa wa Malaria na Maelekezo sahihi kuhusu dhana hizi, Soma zaidi hapa

Hizi hapa ni baadhi ya Dhana Potofu ambazo watu wanazo kuhusu Ugonjwa wa Malaria,na Maelekezo sahihi Kuhusu dhana hizi;

1. Ugonjwa wa Malaria husababishwa Na Mbu,

Hapana! Ugonjwa wa Malaria hausababishwi na mbu,

ila unasababishwa na vimelea wanaojulikana kama PLASMODIUM, na Mbu ni kibebeo tu cha vimelea hivi.

Ugonjwa wa Malaria ni ugonjwa ambao husababishwa na vimelea vya magonjwa viitwavyo Plasmodium.

Vimelea hivi vipo vya aina mbali mbali kama vile; Plasmodium vivax,plasmodium malariae,plasmodium falciparum, plasmodium ovale

Vimelea hivi huenezwa na mbu jike aina ya anofelesi (anopheles). Lakini watu wengi huelewa kwamba malaria husababishwa na mbu. Mbu huyu husaidia katika usambazaji tuu wa vimelea husika.

2. Ukiona unapata maumivu makali ya kichwa,basi utakuwa una Malaria Hivo tumia dawa za Malaria

Hapana sio kweli, Maumivu ya kichwa pekee sio sababu ya kutosha ya kusema mtu ana Malaria hivo aanze dose za Malaria,

Zipo sababu nyingi ambazo huweza kupelekea tatizo la Maumivu makali ya Kichwa,

SOMA ZAIDI HAPA; Chanzo cha Maumivu makali ya Kichwa

MAUMIVU YA KICHWA MARA KWA MARA

3. Ukinywa Pombe zaidi hupati Malaria,

Sio kweli, Ugonjwa huu huweza kuwapata Wote Walevyi na Wasio walevyi

4. Kunywa Dawa Za Malaria kabla ya Kuugua Malaria inakufanya Usiumwe Malaria kabsa,

Wapo baadhi ya watu hutumia Dawa za Malaria wakati hawana Malaria kwa Lengo la kuwakinga, Hasa wale ambao wapo kwenye maeneo yenye mbu sana au Malaria na ni wageni maeneo hayo,

Epuka tabia hii ya kutumia Dawa za Kutibu Malaria wakati huna Malaria,hii itakufanya ujenge tatizo lingine ikiwemo; Hili la Usugu wa Dawa pamoja na vimelea vya magonjwa(Drugs resistance and Antimicrobial resistance),

Tumia dawa za Kutibu Malaria,kama kweli una Ugonjwa wa Malaria.

5. Ugonjwa wa Malaria hautibiki kabsa,

Wapo baadhi ya watu huamini kwamba Ugonjwa wa Malaria hautibiki au hauna Dawa kabsa,hivo Usijihangaishe na matibabu ya Hospitalin,

Ukweli ni kwamba,Malaria inatibika kwa Asilimia 100%,

ila mzunguko wake ni Ule ule, Hata kama umekunywa Dawa za Malaria ukapona, ukikaa Kwa Muda kidogo na ukawa kwenye mazingira ya kung’atwa na Mbu waliobeba vimelea vya malaria(Plasmodium), unaweza Kuumwa tena Ugonjwa huu wa Malaria.

Unachotakiwa kufanya,ni kujikinga Zaidi hasa na Mbu,kwa Njia mbali mbali kama vile;

• Kwa kulala kwenye Neti au chandarua chenye dawa

• Kusafisha mazingira, na kuhakikisha hakuna Maji maji yanayotuama kwenye eneo lako n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.