Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Je mtu ayetumia dawa akipima HIV itaonekana au La?

Je mtu ayetumia dawa akipima HIV itaonekana au La?

Haya ni baadhi ya Maswali kutoka kwa Wafwatiliaji wetu;Samahani naomba kuuliza je mtu ayetumia dawa akipima hiv je itaonekana au la!

SOMA ZAIDI HAPA KUJUA…..!!!!

Kwa Mujibu wa “Aidsmap” Watu wanaotumia dawa za ARVs hawashauriwi kupima ili kuangalia majibu yao kwa kutumia vipimo vya haraka yaani Rapid Tests,

Kutumia Vipimo vya haraka(Rapid tests) kujipima mara kwa mara huwa si sahihi kwa watu wanaoishi na VVU wanaotumia matibabu ya VVU.

Hii haimaanishi kwamba Ukipima kama Unatumia dawa hutapata Majibu,ila baadhi ya tafiti zinaonyesha unaweza usipate majibu sahihi hasa kwa mtu anayetumia dawa za ARVs kwa Muda Mrefu zaidi,

Unaweza Usipate Majibu Sahihi kwa kutumia Njia hii ya Upimaji(Rapid tests), je Kwanini?

Hitilafu hizi zinaweza kuonekana kwa sababu athari ya tiba ya kurefusha maisha kwa Mgonjwa mwenye VVU inaweza kuenea hadi kukandamiza mwitikio wa kawaida wa mfumo wa kinga dhidi ya virusi,

Ili Vipimo hivi vitoe majibu hutegemea kugundua kingamwili za VVU yaani HIV antibodies kama sehemu ya mwitikio wa kinga ya mwili,

lakini mara kwa mara watu wanaotumia DAWA kwa muda mrefu wanaweza kupoteza baadhi ya kingamwili zao(Antibodies). Na Hii haimaanishi kwamba tayari wameshapona UKIMWI,

Kwa sababu hiyo, watu wanaotumia matibabu ya VVU na wanatumia vipimo vya haraka yaani Rapid tests au vipimo hasa vile vinavyotokana na sampuli za maji(oral fluid samples), wanaweza kupokea matokeo hasi ya uongo.

Hili ni jambo la kawaida kwa watu ambao walianza matibabu ya VVU miezi kadhaa au miaka baada ya kuambukizwa. Vipimo vya maabara, vinavyotolewa katika mipangilio ya huduma ya afya, hubakia kuwa sahihi Zaidi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.