Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Madhara Makubwa ya Ukataji wa Miti(Misitu)-Mazingira

Madhara Makubwa ya Ukataji wa Miti(Misitu)-Mazingira,

Moja ya changamoto kubwa Duniani kwa Sasa ni kupambana na madhara yanayotokana na Ukataji wa misitu au Miti(deforestation),

Katika Makala hii tumekuchambulia walau kidogo madhara makubwa ya Ukataji wa Miti kwa binadamu,wanyama, na Mazingira kwa Ujumla.

Haya hapa ni baadhi ya Madhara yanayotokana na Ukataji wa Miti au Misitu;

1.Kwenye Afya(Health)

Kumbuka Misitu ndyo makazi makunywa ya Viumbe mbali mbali ikiwemo wadudu pamoja na wanyama mbali mbali,

Hivo ukataji wa Miti au Misitu,huharibu kabsa Makazi ya viumbe haya,

Hali ambayo husababisha Viumbe haya kuhamia kwenye Makazi ya Binadamu(Watu).

Kadri Viumbe hawa(Wadudu&wanyama) wanavyohamia kwenye Makazi ya watu,ndivo huongeza CONTACTS,

KUMBUKA; Wadudu au wanyama ni miongoni mwa wabebaji wakubwa wa vimelea mbali mbali vya magonjwa,

hivo hali hii ya kuongeza Contacts kati ya Viumbe hawa na binadamu, huweza kusababisha Usambazaji Mkubwa wa vimelea mbali mbali vya Magonjwa,

Hata kupelekea uwepo wa Magonjwa mbali mbali kwa binadamu yaani Zoonotic Diseases.

Pia kuna baadhi ya tafiti zilifanyika Mnamo mwaka 2020 zilionyesha kwamba ukataji wa misitu huongeza uwepo wa Ugonjwa wa Malaria,

Hii ni kutokana na kwamba Mbu huongezeka zaidi(flourish) na kuwepo kwenye makazi ya watu kadri Biodiversity inavyoshuka.

2. Tatizo la mabadiliko makubwa ya Hali ya Hewa(Climatic changes),

Hali ambayo husababisha uwepo wa JOTO kali Pamoja na Ukosefu wa MVUA,

Miti husaidia sana Kubalance Carbondioxide(CO2),

Ukataji wa Miti husababisha Miti kutoa hewa ya CO2 ambayo ilihifadhiwa, Kisha kupelekea Uwepo wa Kiwango kikubwa cha CARBON kwenye Atmosphere,

Hali hii huweza kusababisha tatizo la Greenhouseeffect na Mabadiliko makubwa sana ya Hali ya Hewa.

3. Tatizo la Njaa, kutokana na mabadiliko makubwa ya hali ya Hewa ikiwemo ya ukosefu wa Mvua za kutosha,mafuriko, wadudu na wanyama kushambulia zaidi mazao ya Watu n.k

Ukosefu wa chakula,hupelekea ukosefu wa virutubisho muhimu Mwilini,upungufu wa Kinga Mwili,uwepo wa magonjwa mengi zaidi, na Hata kupelekea Vifo.

4. Mmonyoko wa Udongo(Soil Erosion), Mafuriko N.k

5. Kukauka kwa vyanzo Mbali mbali vya Maji, N.k

KUMBUKA; Miti Ni Uhai, Hakikisha unatunza Misitu kadri Uwezavyo.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.