Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu VVU/UKIMWI pamoja na Majibu Yake

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu VVU/UKIMWI pamoja na Majibu Yake

Haya hapa ni baadhi ya Maswali ambayo watu wengi wamekua wakiuliza Kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) na UKIMWI,

1.Nini maana ya HIV?

HIV-kirefu chake ni human immunodeficiency virus,ikiwa na maana ya kirusi kinachosababisha Upungufu wa Kinga Mwilini,

Tafsiri nyingine Ni vrusi vya Ukimwi yaani VVU

2. Nini maana ya AIDS?

AIDS-kirefu chake ni Acquired Immune Deficiency Syndrome,Ikiwa na Maana ya tatizo la Upungufu wa Kinga Mwilini

Tafsiri nyingine ni UKIMWI

3. Ukimwi Unasabababishwa na Nini?

tatizo la Upungufu wa Kinga Mwilini(AIDS)/UKIMWI husababishwa na Virusi(HIV)

4. Jinsi gani Mtu anaweza kuambukizwa Virusi vya UKIMWI(VVU)?

Unaweza kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Njia mbali mbali ikiwemo;

– Kufanya ngono zembe na muathirika wa Ukimwi

– Kushare/Kushirikiana vifaa vyenye ncha kali kama vile nyembe,sindano n.k na Muathirika wa Ukimwi

– Kuchangiwa Damu ya Mtu ambaye tayari ameathirika n.k

5. Nani yupo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi?

– Mwenye Wapenzi wengi

– Anayefanya Ngono zembe

– Makahaba

– Wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile

– Wanashirikiana vifaa vya Ncha kali kama Sindano,nyembe n.k,

-Mfano wanayojidunga madawa ya kulevyia n.k

6. Ninaweza kumtambua mtu mwenye UKIMWI kwa kumuangalia tu?

Njia sahihi ni kwa kufanya vipimo pekee,

Wapo baadhi ya watu wanaweza kuchukua muda pasipo kuonyesha dalili yoyote kwa Nje ila tayari wanamaambukizi ya virusi vya Ukimwi,

Lakini Pia Mtu ambaye anatumia Dawa za Kurefusha maisha(ARVs) na kufuata mashariti yake inaweza kuwa Vigumu sana kumtambua kama ni muathirika wa Ukimwi.

7. Nitatambuaje kama tayari nimeathirika?

Njia Sahihi ni Kwa Kufanya Vipimo

8. Zipi Ni Dalili za UKIMWI?

Dalili zipo nyingi,tumeelezea kwenye makala ya peke yake,ila kwa ufupi,dalili ni pamoja na;

– Uzito kupungua kwa Kasi Sana,Au mtu kukonda

– Mwili kuchoka sana kupita kiasi

– Mtu kuvimba tezi za shingoni,kwapani,au Sehemu za Siri

– Hamu ya chakula Kupotea kabsa

– Kupata homa za Mara kwa Mara

– Mtu kuharisha mara kwa mara n.k

9. Je ninaweza kupata Ukimwi kwa Kushikana Mikono na Muathirika,kugusana,au Kwa kushirikiana vyombo vya Chakula?

Hapana huwezi kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Kwa Njia kama Hizi,

10. Je mtu anaweza kupata UKIMWI kwa kung’atwa na Mbu?

Hapana,Mbu hawezi kusambaza Virusi vya Ukimwi(VVU)

11. Dalili za UKIMWI zinaweza kuchukua Muda gani kuanza kujitokeza toka siku ya Kwanza ya maambukizi?

Asilimia kubwa Inaweza kuchukua Wiki 2 mpaka 4,Dalili kuanza kujitokeza,

Japo wapo baadhi ya watu huweza kuchukua muda bila Dalili zozote kuanza kujitokeza

12. Vipimo vya Ukimwi Vinachukua muda gani kuanza kuonyesha Majibu?

Hii inategemea na aina ya Vipimo ulivyotumia Kupima,

mfano; Rapid tests ambazo hata watu wengi hujipima wenyewe,Asilimia 98% ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi huweza kuchukua hadi Miezi 3 Kuonekana.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.