Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Maumivu ya jino na tiba yake,Chanzo cha tatizo hili ni nini?

Maumivu ya jino na tiba yake,Chanzo cha tatizo hili ni nini?

Watu wengi wanashida ya kuumwa na Jino, je kipi kinasababisha meno kuuma?

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za Maumivu ya Jino Mara kwa Mara;

1. Meno au Jino kutoboka

2. Meno au Jino kuwa na Mpasuko au cracks,

Na wakati mwingine mpasuko huu hutokea jino linapoanzia(root fracture),hali ambayo inasababisha kuwa vigumu kutambua kama jino lako lina Shida.

3. Meno au Jino kuvunjika kwa sababu mbali mbali kama vile; baada ya kuanguka,kupata ajali,kugongwa na kitu kizito n.k

4. Mtu kuwa na tatizo La Meno kusagana(bruxism), na mara nyingi unaweza usijue hasa ikitokea wakati wa usiku ukiwa umelala,

Hali hii huweza kusababisha maumivu ya taya,meno kuachana na baada ya muda
inaweza kuharibu enamel ya meno yako. Hii huleta maumivu ya jino au Meno

5. Tatizo la Majipu, Kuwa na Jipu kwenye eneo la Jino au Meno

6. Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile bacteria,Virusi n.k,

maambukizi kama sinus infections,Herpes simplex virus n.k huweza kusababisha maumivu makali ya Jino

7. Tatizo la Vidonda kwenye fizi pamoja na Meno au Jino(Canker sores).

8. Kuota Meno(Wisdom teeth), Kama ilivyo kwa watoto wadogo ambapo hulia wakati meno yanaota kwa sababu ya maumivu,

vivyo hivo kwa watu wakubwa huweza kupata maumivu wakati meno ambayo hujulikana kama wisdom teeth yanapoota,

Meno haya ni yale ambayo huota nyuma, mwishoni kabsa mwa taya

Na mara nyingi meno haya huanza kuota ukiwa na umri wa kuanzia miaka 17 mpaka 21.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.