Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
MagonjwaUzazi/Ujauzito

Maumivu ya tumbo wakati wa Ujauzito,chanzo chake ni nini?

Maumivu ya tumbo wakati wa Ujauzito,chanzo chake ni nini?

Wanawake wengi hulalamika tatizo hili la Maumivu ya tumbo wakati wa Ujauzito, je ni hali ya kawaida au ni tatizo?

Fahamu; Asilimia kubwa maumivu haya ya tumbo wakati wa Ujauzito ni kawaida,

Kwenye kipindi cha miezi mitatu ya Mwanzo yaani First trimester (weeks 0 mpaka 12),

nikawaida kwa Mwanamke mjamzito kupata maumivu madogo( mild pains) ya tumbo kwenye eneo la chini ya Tumbo,

Hali hii hutokana na mabadiliko ya vichocheo mwilini pamoja na tumbo linalokua,

JE MAUMIVU YAKIWA MAKALI SANA NI KAWAIDA?

Hii sio kawaida endapo;

• Unapata maumivu makali ya tumbo

• Damu zinaanza kutoka sehemu za Siri

• Maumivu ya tumbo yapo upande wa juu wa tumbo hasa upande wa kulia, hii huweza kuashiria tatizo la kifafa cha Mimba(pre-eclampsia)

• Unapata maumivu wakati wa Kukojoa, joto kuwa juu(Kuwa na Homa), Mkojo kuwa na harufu sana,Kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa n.k,

Hizi huweza kuwa dalili za Maambukizi kwenye njia ya Mkojo yaani UTI.

• pia Maumivu makali ya tumbo wakati wa Ujauzito huweza kuashiria;

– Tatizo la Mimba kutunga Nje ya Kizazi(ectopic pregnancy)

– Mimba kutoka yenyewe(miscarriage)

– Ugonjwa wa UTI

– Maumivu ya tumbo pamoja na kupat a choo kigumu zaidi

– Tatizo la kondo la nyuma kuachia kwa kitaalam hujulikana kama placental abruption

– Kuanza Labour kabla ya Wakati, yaani premature/preterm labour,

Hii hutokea Ujauzito ukiwa haujafikisha wiki 37

– Dalili za kifafa cha Mimba, Maumivu ya tumbo yakiwa upande wa juu wa tumbo hasa upande wa kulia, hii huweza kuashiria tatizo la kifafa cha Mimba(pre-eclampsia),

ambapo huweza kuambatana na dalili zingine kama vile;

1.Kuvimba sana miguu,mikono,Uso n.k,

2. Mama mjamzito kuona marue rue

3. Kupata maumivu makali sana ya kichwa

4. Presha Kuwa Juu

5. Uwepo wa Proteins kwenye mkojo, Mama huyu akifanyiwa vipimo vya Mkojo huona kuna proteins kwenye mkojo wake

6. Kuhisi kichefuchefu na kutapika n.k

• Mtoto kutokusikika akicheza tena,kwa wale ambao ujauzito umefikia umri wa mtoto kuanza kucheza,

Hapa nazungumzia Ujauzito kuanzia wiki ya 20,24 na kuendelea..

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

#Category:Ujauzito

#Tatizo:MAUMIVU YA TUMBO

#Afyaclass:Chanzo chake

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.