Mtoto juu ya Mtoto,Mimba mara tu baada kutoka Kujifungua-Zingatia haya
Mtoto juu ya Mtoto,Mimba mara tu baada kutoka Kujifungua-Zingatia haya
Wanawake wengi baada ya kujifungua husubiri kwanza waone hedhi ndipo waanze kuchukua tahadhari ya kujikinga na Mimba,
Kumbuka hedhi ni matokeo ya kutokuwa na urutubishaji wa Yai, endapo yai limerutubishwa huwezi ona hedhi kama ulivyokuwa unasubiria ndipo uanze kujikinga,
Hii imepelekea wanawake wengi kubeba mimba ambazo hazijapangwa baada ya kujifungua,
Una mimba nyingine na huku bado unanyonyesha,
Kumbuka Pia kwa baadhi ya wanawake huchelewa Sana kupata hedhi yao ya kwanza toka Kujifungua,
Kumekuwa na Ongezeko kubwa la Wanawake ambao wanajikuta Tayari Wana Mimba wakati watoto wao bado ni wachanga kabsa,
Hii huwafanya kuwa na Msongo zaidi wa mawazo hata kupelekea kushindwa kumhudumia vizuri mtoto ambaye tayari kazaliwa.
Wengi wao ukiawauliza,watakuambia Mimi nilikuwa nasubri kupata HEDHI YANGU ndipo niaze kuchukua tahadhari,
Sasa Leo nimekupa elimu hii japo kidogo, Ufahamu kwamba hedhi ikija ujue ni matokeo kwamba yai halijafanikiwa kurutubishwa,
lakini kama mzunguko wako wa hedhi umekaa Sawa,yai likatoka kwenye Vifuko vya mayai(Ovaries), Kisha ukafanya mapenzi bila tahadhari yoyote,unaweza kabsa kupata Ujauzito na Swala la kuona hedhi isilione kabsa,
JIKINGE NA MIMBA AMBAZO ZIPO NJE YA MPANGO