Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Muda Mzuri na Sahihi wa Kufanya Mazoezi,Je muda upi ni mzuri kwa ajili ya mazoezi?

Muda Mzuri na Sahihi wa Kufanya Mazoezi,Je muda upi ni mzuri kwa ajili ya mazoezi?

Kama wewe ni mtu wa mazoezi,bila shaka unaweza kujiuliza Swali hili,ni muda upi sahihi na Mzuri wa Kufanya mazoezi?

Swali hili linaweza kutegemea pia aina ya kazi au Majukumu unayokuwa nayo kila siku,

Na wataalam wengine,wanaweza kujibu swali hili kwa kusema; Muda mzuri wa kufanya mazoezi ni wakati wowote unapokuwa na muda wa kufanya hivo,

Na ni bora kufanya Muda wowote unaopata,kuliko kutokufanya kabsa.

Kutokana na tafiti mbali mbali,Kuna muda Sahihi au Mzuri zaidi kwa ajili ya kufanya MAZOEZI,

Wakati unapanga kufanya Mazoezi kwa Ufasaha kabsa, zingatia sheria hii(FITT Principle), na hapa tunaangalia;

•F-Frequency

• I-Intensity

• T-Time

• T-Type

Sasa katika makala hii,sisi tunaangalia kipengele kimoja cha TIME, na tumejikita zaidi kuhusu Muda sahihi au Mzuri kwa ajili ya kufanya Mazoezi,

JIBU: Muda Sahihi wa Kufanya Mazoezi ni pale unapokuwa na Muda wa Kufanya hivo, ila Kuna faida zaidi za Kufanya Mazoezi wakati wa ASUBUH pamoja na JIONI,

FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI ASUBUHI

– Kufanya mazoezi asubuhi husaidia kupunguza uchovu,mwili kurelax na kuongeza Uzalishaji kwa siku nzima,

ikiwa na maana hata kazi zako za siku utafanya kwa ufanisi mkubwa sana kama ulifanya mazoezi asubuh ndipo ukajiandaa kwenda kufanya kazi zako.

Kuna utafiti mmoja ulifanyika ambapo wahusika walikuwa vijana 51 wenye afya, Wahusika hawa walifanya mazoezi Kwa Dakika 30 kila sku asubuh kwa siku 3 ndani ya wiki moja, na matokeo yake yalikuwa hivi;

• Hata kulala kwao usiku kulikuwa kuzuri zaidi

• Msongo wa mawazo kuondoka,mwili kurelax na kuwa na mood

• Ufanisi wa kazi za siku nzima uliongezeka

• Na pia Swala la kuwa na Usingizi wakati wa mchana lilipungua zaidi.

Hii ni ikilinganishwa na group lingine ambalo halikufanya mazoezi yoyote yaani Control group kwenye utafiti.

– Pia kutokana na kwamba, kiwango cha cortisol kinaweza kuwa kikubwa wakati wa asubuh, kufanya mazoezi wakati huu wa asubuh huweza kusaidia mtu kupata matokeo mazuri zaidi,

CHANGAMOTO ZA KUFANYA MAZOEZI ASUBUH

– Kutokupata muda wa kutosha wa kulala,kwani lazima uanze mazoezi mapema,ili umalize ujiandae kwenda kazini,

Hii ni changamoto kubwa kwa watu wengi, na kutokana na hofu ya kuchelewa kazini,wengi mazoezi ya asubuh wanafanya wakiwa wapo mapumziko na sio siku za kazi, hasa kwa wale ambao kazi zinawahitaji kudamka sana asubuh.

– Baadhi ya tafiti zinaonyesha mazoezi ya asubuhi yanaweza kupunguza hamu ya kula siku nzima,

Hii huweza kutokea hasa ukifanya mazoezi ya juu au kupita kiasi(High intensity exercise)

FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI WAKATI WA JIONI

– Faida ya kwanza ni mtu kuwa na muda wa kutosha wa kufanya Mazoezi,

Mara nyingi mtu anayefanya mazoezi yake jion,hupata muda zaidi wa kufanya mazoezi kuliko asubuh,

Na hii humfanya mhusika kufocus zaidi kwenye mazoezi,kichwa kurelax na kufanya mazoezi vizuri zaidi.

– Baadhi ya tafiti zinaonyesha pia,kufanya mazoezi jioni husaidia kuboresha Usingizi wako wakati wa usiku,

Lakini pia mazoezi yanayofanywa wakati wa jion hayawezi kupelekea tatizo la mtu kukosa hamu ya chakula

mazoezi ya nguvu ya juu hayaathiri usingizi au hamu ya kula ikiwa hufanywa mapema jioni.

– Pia huweza kusaidia kuongeza ufanisi wa kazi kama ilivyo ukifanya wakati wa asubuh,

CHANGAMOTO YA KUFANYA MAZOEZI WAKATI WA JIONI

– Kuathiri Usingizi wako, mbali na kwamba kufanya mazoezi wakati wa jion husaidia kuboresha usingizi wako,

Ukifanya mazoezi kwa kiwango cha juu sana na kwa kuchelewa zaidi, na kukosa muda wa kutosha wa mwili kupumzika kabla ya kulala,inaweza kusababisha matatizo kwenye usingizi pia,

Tafiti zinaonyesha,ikiwa umefanya mazoezi kwa kiwango cha juu halafu ukaenda kulala chini ya muda wa Saa Moja toka ufanye mazoezi,unaweza usipate usingizi mzuri,ukachelewa sana kupata usingizi n.k

Hivo unashauriwa kufanya mazoezi jion ila mapema, ili mwili upate muda wa kutosha kwa ajili ya kupumzika kabla ya kwenda kulala.

#Mazoezi:TIME

#WorkOut

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.