Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ripoti Mpya:Ongezeko la Kiwango cha Ukinzani kwa Bacteria wengi hali ambayo hufanya vigumu kuwatibu

Ripoti Mpya:Ongezeko la Kiwango cha Ukinzani kwa Bacteria wengi hali ambayo hufanya vigumu kuwatibu,

Kwa Mujibu wa Shirikila la Afya Duniani(WHO), Kumekuwa na Ongezeko Kubwa la Ukinzani(Resistance) kwa Vimelea wa Magonjwa kama Bacteria,

hali ambayo hutishia Maisha zaidi kwa Sababu ya Bacteria hawa kusababisha maambukizi hatari zaidi kwenye damu ambayo huwa vigumu kuyatibu.

Na hii hupelekea pia Ugumu wa Kupata Tiba na Kupona kwa Wagonjwa, kwani bacteria hawa hawatibiki tena kwa dawa ambazo hapo awali zilikuwa zinasaidia kutibu,

Kwa Mara ya Kwanza kabsa, Ripoti ya “the Global Antimicrobial Resistance pamoja na Use Surveillance System (GLASS)” inatoa Uchambuzi juu ya Kiwango cha Ukinzani wa vimelea hawa yaani antimicrobial resistance (AMR) rates kulingana na tafiti zilizofanywa na kugusa eneo la kitaifa zaidi.

Tafiti zinaonyesha Kwamba; Zaidi ya asilimia 50% ya Ukinzani huu Ulionekana kwa Bacteria ambao husababisha mara kwa mara maambukizi kwenye Damu(Bloodstream infections) mfano ni Klebsiella pneumoniae pamoja na Acinetobacter spp.

Lakini Pia utafiti Ulionyesha Zaidi ya Asilimia 60% ya Neisseria gonorrhoea ambao husababisha Ugonjwa wa Kisonono(Gono) walionyesha Ukinzani Juu ya DAWA jamii ya ciprofloxacin,

Na zaidi ya Asilimia 20% ya Bacteria wa Escheria Coli(E.coli), ambao ndyo kwa kiwango kikubwa husababisha maambukizi kwenje njia ya Mkojo yaani UTI(urinary tract infections)–Walionyesha Ukinzani juu ya Dawa jamii ya ampicillin na co-trimoxazole

Pia hata kwa dawa jamii ya fluoroquinolones.

Ongezeko la Ukinzani huu Limeonekana zaidi kwa angalu asilimia 15% Ukilinganisha na Mwaka 2017, ambapo Ongezeko hili limeonekana zaidi kwa Bacteria wanaosababisha maambukizi kwenye damu(bloodstream infections),

Kama vile;Neisseria gonorrhoea, Escherichia coli pamoja na Salmonella spp.

Na Tafiti zaidi zinahitajika Kujua nini chanzo hasa, Je Janga la COVID-19 linachangia au La! Majibu yote haya yanahitaji Tafiti zaidi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.