Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Ukatili wa Kijinsia:Wadau tuungane kutokomeza hili, tungefanya tathimini ya wapi pa kupeleka rasilimali na nguvu kutokana na uhitaji

Ukatili wa Kijinsia:Wadau tuungane kutokomeza hili, tungefanya tathimini ya wapi pa kupeleka rasilimali na nguvu kutokana na uhitaji,

Unachotakiwa Kujua,Swala la Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia sio Swala la Mtu mmoja,wote tunawajibu wa kupambana na kushinda Vita hii.

Mnamo Tarehe 10,Desemba,2022 ilikuwa ni siku rasmi kwa Ajili ya Maadhimisho ya Kitaifa ya HAKI ZA BINADAMU,

Pamoja na Kuhitimisha KAMPENI YA SIKU 16 kwa ajili ya Kupinga UKATILI WA KIJINSIA, ambapo maadhimisho haya yalifanyika kwenye Mkoa wa DAR ES SALAAM.

Kwenye Maadhimisho hayo,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima alisema;

“Wadau tuungane kutokomeza hili, tungefanya tathimini ya wapi pa kupeleka rasilimali na nguvu kutokana na uhitaji basi eneo hili ndiyo lingehitaji uwekezaji mkubwa kwani ndiyo linaongoza kwa uvunjifu wa haki za binadamu”

Wadau hao Ni Pamoja na;

-SMAUJATA,

– NGOs

– KAMATI ZA MTAKUWWA

– GIRLS GUIDE

– SKAUTI

– REDCROSS

– MABARAZA YA WAZEE NA WATOTO,

– MITANDAO YA WANAWAKE

– TAASISI ZA KIVYAMA HUSUSANI WANAWAKE, VIJANA NA WAZAZI,

– VIONGOZI WA DINI NA WENGINE WOTE KWA UJUMLA.

Waziri Dkt. Gwajima Anasema;

“Ninatangaza vita endelevu dhidi ya wote wanaojihusisha na matendo ya ukatili wa aina hii kwamba wasalimu amri”.

• Kumbuka..!!!!

Haya ni miongoni mwa matukio ya ukatili kwa watoto ambayo yanatokea kwa wingi,

Hizi ni Takwimu ambazo zilitolewa Na Dkt. Gwajima Kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika “Mikoa ya kipolisi inayoongoza kwa ukatili ni Arusha (808), Tanga (691), Shinyanga (505), Mwanza (500) na Ilala (489)

na makosa yaliyoongoza kwa idadi kubwa ni ubakaji (5,899), mimba kwa wanafunzi (1,677) na ulawiti (1,114)”

Ukatili huu ni wakupiga vita sana, na kila mmoja analojukumu la kuhakikisha vitendo hivi havitokei,

maana leo kwa jirani kesho ni kwako, je utakuwa kwenye hali gani endapo ukatili huu umetokea ndani ya Familia yako?

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.