Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kwanini Unashauriwa kuchangia Damu sio chini ya Wiki 12 Toka kuchangia?

Kwanini Unashauriwa kuchangia Damu sio chini ya Wiki 12 Toka kuchangia?

Fahamu ni Salama kabsa Kwa Mwanaume kuchangia damu kila baada ya Miezi 3(wiki 12) Bila kupata shida yoyote,

Na mwanamke ana uwezo wa kuchangia damu kila baada ya Miezi 4 bila shida yoyote,

Muda huu kwa Mwanamke umeongezwa kidogo kutokana na hali ya Mwanamke kupoteza Damu kwa kila mwezi kwenye kipindi cha hedhi.

Kuchangia Damu karibu karibu zaidi yaani kwenye kipindi cha chini ya wiki 12 toka uchangie damu awamu iliyopita huweza kusababisha matatizo kama vile Upungufu wa Madini chuma kwa Mchangiaji damu (iron deficiency),

Wakati wa uchangiaji Damu, Seli nyekundu za damu(Red blood Cells) huondoa Madini Chuma Mwilini,

Na madini haya ni component muhimu sana kwa hemoglobin.

Hata hivo Wataalam wa afya hushauri zaidi kula Mlo wenye Madini Chuma ili kupata madini haya zaidi kwa Mchangiaji Damu,

Moja ya Sababu kwa Mchangiaji Damu Kushauriwa kuchangia damu Kila baada ya wiki 12 na kuendelea na sio chini ya hapo,

Ni ili kuepuka kupata tatizo la Upungufu wa Madini chuma Mwilini(Iron deficiency) kwani Tunajua inachukua muda kwa mwili kunyonya tena madini chuma ili kutengeneza chembe chembe hizo nyekundu mpya.”

Hivo basi ni Vizuri pia Kwa Mchangiaji Damu kupewa elimu juu ya Vyanzo mbali mbali vya Madini Chuma, ili kusaidia kurudisha Madini hayo ambayo hupotea mwilini wakati wa uchangiaji damu.

KUCHANGIA DAMU HAKUNA MADHARA(soma hapa)

Watu wengi au jamii nyingi zimekuwa zikishikilia dhana potofu kwamba uchangiaji damu una madhara makubwa mwilini,

na mtu akichangia damu itamlazimu kufanya hivyo kila mara.

DHANA POTOFU KUHUSU UCHANGIAJI DAMU

-Mtu akichangia damu itasababisha damu kuongezeka kila mara na kumlazimu kutoa damu kila wakati kwenye maisha yake yote.

Dhana hii ni potofu na imekuwa ikiwapa shida sana watu wanaohamasisha mpango wa uchangiaji Damu Salama.

FAHAMU HILI; Kulingana na maumbile ya Mwanaume yalivyo, Mwanaume ana uwezo wa kuchangia damu kila baada ya Miezi 3 Bila kupata shida yoyote,

Na mwanamke ana uwezo wa kuchangia damu kila baada ya Miezi 4 bila shida yoyote.

Kama mtu ana shida ya damu kuongezeka akutane na wataalam wa maswala ya Damu kuangalia kwanini chembe chembe zake za damu zinajizalisha kupita kiasi na kupata Tiba sahihi,

Lakini atambue hakuna uhusiano wa kuchangia damu na damu kuongezeka kwa wingi.

Vitu ambavyo huzingatiwa wakati wa uchangiaji damu ni pamoja na Kupima Uzito wa mwili, Presha N.K.

EPUKA IMANI POTOFU CHANGIA DAMU OKOA MAISHA.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.