Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

PICHA:Hii ni chain inayoonyesha Wanawake ambao wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi(Cervical Cancer)

PICHA:Hii ni chain inayoonyesha Wanawake ambao wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi(Cervical Cancer)

SARATANI NI NINI?

Saratani ni hali ya ukuaji wa seli hai za mwili usio wakawaida au uliozidi kiwango(overgrowth/abnormal cells growth)

,Kwahyo basi, Saratani ya shingo ya kizazi ni ukuaji usio wa kawaida wa seli hai zilizopo au zinazounda eneo la shingo ya kizazi

Wanawake ambao wapo Kwenye Hatari ya Kupata saratani ya Mlango wa Kizazi,

Kwa Ujumla wanawake wote wapo kwenye hatari ya Kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi, ila kundi hili hapa Chini Lipo kwenye hatari zaidi.

KUNDI LILILOPO KATIKA HATARI YA KUPATA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

➖ Wanawake wanaoanza kushiri tendo la Ndoa au mapenzi wakiwa na umri mdogo mfano kabla ya miaka 18 au 20.

➖ Wanawake wenye wapenzi wengi yaani Multiple sexual parteners

➖ Wanawake wenye Umri mkubwa mfano miaka 50 na kwenda mbele,

Saratani hii huweza kuathiri zaidi Wanawake Kuanzia Miaka 35 mpaka 49

➖ Wanawake wanaozaa katika umri mkubwa mfano miaka 48.

➖ Wanawake wanaotumia dawa zozote zinazohusu kuongeza uzalishaji wa seli hai za Mwili.

➖ Wanawake Wenye Maambukizi ya Ukimwi(HIV/AIDS) au wanawake wenye magonjwa yoyote ambayo huweza kuathiri mfumo wa Kinga ya Mwili

➖ Wanawake wanaoshambuliwa na Kirusi cha Human papilloma virus(HPV) mara kwa mara

➖ Wanawake wanaovuta Sigara

➖ Wanawake wanaozaa watoto wengi

➖ Wanawake wanaotumia vidonge vya Uzazi wa Mpango(birth control Pills) Kwa Muda Mrefu zaidi, Mfano Kwa Miaka 3,5 au Zaidi

– Wanawake wanaoolewa mapema na Kuanza kuzaa mapema sana wakiwa bado wadogo(Early Marriage&Early child birth)

– Kuwa na historia ya tatizo hili Kwenye Familia yako. N.k

SOMA ZAIDI HAPA..!!!

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.