Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la Misuli Kukaza(Muscle cramps),chanzo,dalili,na Tiba yake

Tatizo la Misuli Kukaza(Muscle cramps),chanzo,dalili,na Tiba yake

Muscle cramp ni tatizo la Misuli kukaza pasipo wewe kupanga yaani muscle involuntary contraction, huku hali hii ikiambatana na maumivu makali,

Tatizo hili huweza kuhusisha aina moja ya msuli kukaza au zaidi ya Msuli mmoja na hutokea kwa muda tu,

Msuli huweza kukaza gafla na kukusababishia maumivu makali

DALILI ZA TATIZO HILI LA MISULI KUKAZA(MUSCLE CRAMPS)

Mara nyingi tatizo hili la Misuli Kukaza hutokea MIGUUNI hasa kwenye eneo la calf,

Tatizo hutokea gafla, huku misuli kukaza ikiambatana na Maumivu makali kwenye eneo tatizo lilipotokea,

Na wakati mwingine unaweza kuhisi au kuona kitu kigumu ambacho ni mkusanyiko wa Tissues za misuli iliyokakamaa chini ya Ngozi yako.

Kwa kawaida tatizo hili la Misuli Kukaza yaani Muscle cramps hutokea kwa Muda tu kisha huisha Lenyewe,

Ila Nenda hospital mapema kupata Msaada endapo;

  • Tatizo hili hutokea kila mara
  • Tatizo hili hukusababishia madhara zaidi(severe discomfort)
  • Tatizo hili huambatana na Miguu kuvimba,Ngozi kubadilika na kuwa nyekundu n.k
  • Tatizo hili huambatana na misuli kuwa dhaifu na kukosa Nguvu hata baada ya kuisha
  • Hali kutokubadilika hata baada ya kujihudumia mwenyewe n.k

CHANZO CHA TATIZO HILI LA MISULI KUKAZA(MUSCLE CRAMPS)

– Msuli au Misuli kutumika kupita kiasi, Mfano kwa Wachezaji wa Mpira huweza kutokewa na tatizo hili la Misuli kukaza(muscle cramps) mara kwa mara

– Upungufu wa Maji Mwilini(dehydration)

– Msuli kukaa sehemu moja au kubanwa sehemu moja kwa Muda Mrefu

– Na Wakati mwingine tatizo hili hutokea Kwa Gafla pasipo kujua Sababu halisi ni ipi.

Kwa Asilimia kubwa misuli kukaza hakuhusishwi na tatizo lolote kubwa kiafya, ila wakati mwingine huweza kuwa na uhusiano wa karibu na matatizo haya;

  1. Kutokuwa na Mzunguko mzuri wa Damu yaani Inadequate blood supply kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo mishipa ya arteries inayopeleka damu miguuni kuwa mywembamba zaidi, tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Extremities arteriosclerosis, Ingawa tatizo hili huisha mara moja baada ya mtu kuacha kufanya mazoezi.
  2. Tatizo la Nereves kubanwa yaani Nerve compression hasa eneo la Uti wa mgongo
  3. Upungufu mkubwa wa madini mwilini kama vile potassium, calcium au magnesium

SABABU HIZI HUONGEZA HATARI YA WEWE KUPATA TATIZO HILI LA MISULI KUKAZA(MUSCLE CRAMPS)

1. Umri kuwa Mkubwa zaidi

2. Kuwa na Upungufu mkubwa wa Maji Mwilini

3. Kuwa Mjamzito, tatizo hili pia huweza kutokea mara kwa mara Kwa wakina mama Wajawazito

4. kuwa na matatizo mengine kiafya kama vile; ugonjwa wa kisukari,matatizo ya Neva,Ini au matatizo kwenye Tezi la Thyroid

JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI(KINGA&TIBA)

✓ Hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku

✓ Epuka kufanya Mazoezi kupita kiasi, au epuka kutumia misuli kupita kiasi

✓ Nyoosha Misuli yako kabla na baada ya kutumia msuli wowote kwa muda mrefu(muscles stretching) n.k.

SOMA HAPA:Baadhi vya vyakula vya kutumia kama una tatizo hili la Misuli kukaza(Muscle cramps)

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.