Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la Sore throat,chanzo,dalili na Tiba yake

Tatizo la Sore throat,chanzo,dalili na Tiba yake

Tatizo la Sore throat kwa jina lingine hujulikana kama Pharyngitis,

Tatizo hili huhusisha mtu kupata maumivu kooni/koo kuuma, au hali ya muwasho au Irritation kooni ambapo huweza kutokea wakati wa kumeza kitu au hata ukiwa humezi kitu chochote,

DALILI ZA SHIDA YA SORE THROAT KWA MTU

Dalili zake huweza kutofautiana kulingana na chanzo chake, ila kwa ujumla shida hii huweza kuhusisha dalili kama vile;

– Kupata Maumivu Kooni

– Maumivu kooni kuzidi wakati wa kumeza kitu chochote au wakati wa kuongea

– Kupata shida ya kumeza kitu chochote

– Kuvimba kwa tezi za shingoni

– Mtu kupata tonses ambapo wakati mwingine huonekana kama na Usaha kwa ndani

– Sauti kukauka n.k,

Maambukizi yoyote ambayo husababisha shida hii,huweza kuleta pia;

• Homa kwa mgonjwa

• Mgonjwa kupata kikohozi

• Shida ya Pua kuvimba au Runny nose

• Mtu kupiga chafya sana

• Kupata maumivu ya kichwa

• mwili mzima kuuma

• kuhisi kichefuchefu na kutapika n.k

CHANZO CHA TATIZO HILI LA SORE THROAT

1. Maambukizi yanayotokana na Viruses,

– kama vile Virusi wanaosababisha mafua au homa ya Mafua(Cold/Flu)

Common cold

Flu (influenza)

Mono (mononucleosis)

Measles

Chickenpox

Coronavirus (COVID-19)

Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(HIV/AIDS) n.k

2. Maambukizi yanayotokana na Bacteria,

Maambukizi mengi yanayotokana na bacteria huweza kusababisha shida hii ya Sore throat,

Hasa hasa Bacteria jamii ya Streptococcus pyogenes (group A streptococcus)

3. Sababu zingine ni kama vile;

-Shida ya mzio/allergies

– Shida ya Ukavu hasa wa hewa unayovuta yaani Dry indoor air

– Kupumulia Mdomo kutokana na shida kama vile chronic nasal congestion

– Uvutaji wa Sigara,tumbaku au kemikali zozote ambazo huweza kusababisha Irritation kooni

– Tatizo la acid reflux au Gastroesophageal reflux disease (GERD) n.k.

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

– Watoto wenye umri wa miaka 3 mpaka watu wenye umri wa miaka 15

– Watu wanaovuta sigara au tumbaku

– Wenye shida ya Allergies/Mzio hasa kwa vitu kama vile vumbi n.k

– Wenye kinga ya Mwili Dhaifu kama vile;

• Wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi

• Wagonjwa wa Kisukari

• Wanaopata tiba kama vile chemotherapy

• Wenye msongo wa mawazo

• Wanaopata Lishe Duni n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

Tiba ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake

Hivo kama ni viral Infection,bacterial Infection, n.k basi utapata tiba kulingana na vitu hivi,

Ila kwa upande wa kupunguza maumivu na homa tumia dawa kama vile acetaminophen,ibuprofen n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.