Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Unaweza Kupata Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI hata kama uliyefanya naye Mapenzi umempima yupo NEGATIVE

Unaweza Kupata Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI hata kama uliyefanya naye Mapenzi umempima yupo NEGATIVE,

Ni dhahiri kwamba Watu wengi hivi Sasa wanadhana kwamba,

ili niwe Salama nikitaka kufanya Mapenzi lazima tupime na kama tupo Negative basi tupo Salama tunaweza fanya Mapenzi bila hata kinga,

Unachotakiwa Kujua ni kwamba kufanya ngono Zembe eti kwa Sababu mmepima kwa mara ya kwanza mpo Negative ni hatari zaidi kwako kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi(VVU).

Je ni kwanini hili huweza kutokea? soma hapa

Kuna vitu hivi viwili vya Muhimu sana unatakiwa kujua,

(1) window period

(2) Incubation Period

• Window Period- hapa tunazungumzia kipindi toka unapata maambukizi ya Ugonjwa mpaka kipimo kinaposoma,

Ambapo kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi huweza kuchukua mwezi mpaka miezi 3 kulingana na mwili au kinga ya mwili wa mhusika,

fahamu kwamba ili kipimo kisome lazima mwili wako utengeneze Antibodies ambapo kwa asilimia kubwa huweza kuchukua kipindi hiki cha chini ya mwezi mmoja mpaka miezi 3,

Ndyo maana ukipima hospital unashauria kurudi baada ya miezi 3 ili kuangalia mwili wako kama bado haujatengeneza hizi antibodies.

Maana yake mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi akiwa kwenye kipindi hiki cha kabla ya mwili kutengeneza hizi antibodies hata ukimpima atatoa majibu Negative,

Hivo basi ukishiriki naye tendo kwa kipindi hiki kwa vile unaona yupo negative,ndyo unakuwa kwenye hatari zaidi kwani ni kipindi ambacho virusi hujizalisha kwa kasi zaidi na kushambulia mwili,wakati huo huo mwili wako bado haujatengeneza kinga ya kupambana na maambukizi haya.

• Wakati Incubation Period- Tunazungumzia kipindi toka kupata maambukizi ya Ugonjwa mpaka mwili kuanza kuonyesha dalili,

ambapo kwa Maambukizi ya Virusi vya Ukimwili kutegenemea na mwili wa mhusika huweza kuchukua kipindi cha wiki Moja, Mwezi,Na kuendelea kulingana na mwili wa mhusika.

Hivo basi Kufanya Ngono zembe eti baada ya kumpima mtu kwa mara ya kwanza yupo Negative bado ni hatari zaidi kwako,

Usalama unakuwepo endapo mmepima na kurudia baada ya kipindi cha Window Period, maana hapa ndyo Hali ya kweli ya maambukizi ya Virusi hivi vya Ukimwi Hujulikana kwa wahusika.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.