Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Athari za ukeketaji kwa wanawake,elimu kuhusu ukeketaji

Athari za ukeketaji kwa wanawake,elimu kuhusu ukeketaji

Pata Elimu kuhusu ukeketaji,athari zake au Changamoto zake,Soma zaidi hapa

• • • • •

MADHARA YA UKEKETAJI KWA MWANAMKE(Hii ni mojawapo ya mila potofu)

Hii ni mojawapo ya mila potofu ambayo ni hatari kwa afya ya mwanamke. Kitendo hiki huhusisha kukata au kupunguza baadhi ya sehemu katika utupu(uke) wa mwanamke ikiwemo kisimi,mashavu ya uke N.K

Ambapo jamii zinazofanya kitendo hiki zikiamini kwamba eti kinamsaidia mwanamke kutokuwa na tabia mbaya kama umalaya N.k na kuweza kutulia katika ndoa yake. Lahasha! hyo sio dawa.

MADHARA YA UKEKETAJI KWA MWANAMKE NI PAMOJA NA;

• Mwanamke kuvuja damu nyingi wakati wa ukeketaji na kupata shida ya kuishiwa na damu

• Mwanamke kuchanika vibaya wakati wa kujifungua na kupoteza damu nyingi zaidi

• Mwanamke kupata maumivu makali wakati wa kufanyiwa kitendo hiki

• Mwanamke kupoteza maisha wakati anafanyiwa ukeketaji au wakati anajifungua kutokana na kumwaga damu nyingi sana

• Mwanamke kuathirika kisaikolojia na kujiona yuko tofauti na wanawake wenzake hasa akiangalia maumbile yake

• Mwanamke kupatwa na magonjwa mengine kwa haraka kwani kwa asilimia kubwa kitendo hiki hakifanyiki katika mazingira ya Usafi

EPUKA UKATILI HUU KWANI HAUNA FAIDA YOYOTE KIAFYA,BADALA YAKE NI CHANZO CHA MADHARA MAKUBWA KIAFYA IKIWEMO PAMOJA NA KUPOTEZA MAISHA YA WATU.

 

BONUS TIPS:TOHARA KWA WANAUME

Baadhi ya jamii bado hazijafahamu faida za wanaume kufanyiwa tohara na hasara kubwa ambazo huweza kutokea kwa wanaume ambao hawajafanyiwa tohara. katika makala hii tumechambua faida za mwanaume kufanyiwa tohara kama ifuatavyo;

FAIDA KWA MWANAUME MWENYEWE BAADA YA KUFANYIWA TOHARA NI PAMOJA NA;

– Mwanaume aliyetahiriwa huwa rahisi zaidi kujisafisha na kuondoa uchafu wote kwenye ngozi ya uume wake

– Mwanaume kutahiriwa hupunguza sana maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo yaani Urinary tract infection(UTI)

– Mwanaume kutahiriwa hupunguza sana maambukizi ya magonjwa mbali mbali ya zinaa yaani Sexual transmitted diseases(STD’s)

– Mwanaume kutahiriwa hupunguza matatizo mbali mbali kwenye uume kama vile tatizo la phimosis ambalo huweza kusababisha ngozi ya mbele ya uume(foreskin) au kichwa cha uume kuvimba

– Mwanaume aliyetahiriwa huweza kufanya tendo la ndoa vizuri zaidi kuliko mwanaume ambaye hajatahiriwa

– Mwanaume kutahiriwa hupunguza tatizo la kansa ya uume yaani penile cancer n.k

FAIDA KWA MWANAMKE AMBAYE YUPO KIMAHUSIANO NA MWANAUME AMBAYE AMEFANYIWA TOHARA

• Mwanamke anayeshiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye katahiriwa huridhika kwa urahisi zaidi kuliko mwanamke ambaye hushirki tendo la ndoa na mwanaume ambaye hajatahiriwa,

Hii ni kwa sababu mwanaume aliyetahiriwa uume wake huweza kusimama kwa muda mrefu zaidi na kuwa na hamasa ya kurudia tendo mara nyingi zaidi kuliko mwanaume ambaye hajatahiriwa

• Mwanamke anayeshiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye katahiriwa huwa katika hatari ndogo zaidi ya kushambuliwa na magonjwa mbali mbali ya zinaa(STD’s) kuliko mwanamke ambaye hushirki tendo la ndoa na mwanaume ambaye hajatahiriwa,

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba; Maambukizi ya kirusi cha Human papilloma virus(HPV),genital herpes,kaswende(syphillis), Trichomoniasis pamoja na maambukizi ya HIV hupungua zaidi endapo tendo la ndoa linafanyika na mwanaume akiwa ametahiriwa kuliko ambaye bado hajatahiriwa.

• Mwanamke anayeshiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye katahiriwa yupo kwenye hatari ndogo ya kupatwa na saratani ya mlango wa kizazi(cervical cancer) kuliko mwanamke ambaye hushirki tendo la ndoa na mwanaume ambaye hajatahiriwa,

• Mwanamke anayeshiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye hajatahiriwa yupo kwenye hatari ya kuingiziwa uchafu kutoka kwa mwanaume,kushambuliwa na vimelea vya magonjwa kama vile bacterial vaginosis,yeast infection, pamoja na kushindwa kubalance kiwango cha PH ukeni, kuliko mwanamke ambaye hushirki tendo la ndoa na mwanaume ambaye katahiriwa

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

[sc_fs_multi_faq headline-0=”h3″ question-0=”Aina za Ukeketaji ni Zipi?” answer-0=”Hizi ni baadhi ya aina za Ukeketaji,Type I – Clitoridectomy,Aina hii huhusisha kuondoa Kinembe yaani Partial or total removal of the clitoris, Aina Zingine ni Pamoja na;Type II – Excision,Type III – Infibulation Pamoja na Type IV, Hizi ndizo baadhi ya aina za Ukeketaji.” image-0=”” headline-1=”h3″ question-1=”Madhara ya Ukeketaji kwa Wanawake” answer-1=”Moja ya madhara ya Ukeketaji kwa Mwanamke ni pamoja na Mwanamke kuvuja damu nyingi wakati wa ukeketaji na kupata shida ya kuishiwa na damu, Mwanamke kuchanika sana na kuvuja damu nyingi wakati wa Kujifungua n.k.” image-1=”” headline-2=”h3″ question-2=”Faida ya Tohara kwa Mwanaume ni Ipi?” answer-2=”Moja ya Faida kubwa ya Mwanaume kutahiriwa ni pamoja na Mwanaume aliyetahiriwa huwa rahisi zaidi kujisafisha na kuondoa uchafu wote kwenye ngozi ya uume wake,Kujikinga na magonjwa mbali mbali ikiwemo Saratani n.k” image-2=”” count=”3″ html=”true” css_class=””]

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.