Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kuumwa kichwa baada ya Mazoezi na Vitu vya kufanya

Kuumwa kichwa baada ya Mazoezi na Vitu vya kufanya

Je unasumbuliwa na tatizo la maumivu ya kichwa baada ya kufanya mazoezi?

Baadhi ya watu hupatwa na tatizo hili mara kwa mara, na hizi hapa ni baadhi ya dalili ambazo huweza kujitokeza;

– Kupata Maumivu ya shingo pia

– Kupata Maumivu kwa upande mmoja au pande zote mbili za kichwa

– Kuhisi kichwa kama kinagonga

– Mishipa ya damu pembeni ya kichwa kucheza cheza sana na kupata maumivu

– Wakati mwingine maumivu ya kichwa huwa kama ya kipandauso na kuhusisha athari kwenye kuona

HIZI NI BAADHI YA MBINU ZA KUKUSAIDIA KAMA UNAPATA SHIDA HII

1. Epuka kufanya mazoezi katika hali ya joto sana au baridi sana.

2. Usifanye mazoezi kupita kiasi ambacho umezoea,fanya kwa kiasi

3. Hakikisha unakunywa maji mengi ili uwe na maji ya kutosha mwilini.

4. Pata mapumziko ya kutosha kila siku, ikiwa ni pamoja na saa nane za kulala.

5. Badilisha utaratibu wako wa mazoezi. Jaribu aina nyingine ya shughuli na uone ikiwa inasababisha maumivu ya kichwa au la!.

6.Pata muda wa kuPasha joto mwili na muda wa kuacha mwili upoe vizuri, pamoja na kujenga nguvu polepole baada ya muda.

7. Wakati mwingine unashauriwa kuvaa vitu kama miwani ya jua ikiwa nje pana mwanga mkali sana na nguo zinazonyonya unyevu ikiwa ni joto sana.

8. Kula lishe bora, na epuka vyakula vilivyosindikwa zaidi,

Pata pia matunda mbali mbali kama vile tikiti maji,tango,embe,parachichi,papai bila kusahau mboga za majani.

9. Tumia Dawa za kutuliza maumivu Kama Panadol, ila kama shida ni endelevu,nenda hospital kwa Uchunguzi zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

[sc_fs_multi_faq headline-0=”h3″ question-0=”Je ni muda gani sahihi wa kufanya mazoezi?” answer-0=”Fanya mazoezi kulingana na ratiba yako,ila muda mzuri zaidi wa kufanya mazoezi ni asubuh na Jioni. Jitahidi kufanya mazoezi angalau kwa dakika 30(nusua saa) Kila siku.” image-0=”” headline-1=”h3″ question-1=”Je mazoezi ni Tiba?” answer-1=”Ndyo,mbali na mazoezi kusaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwili,kutukinga na magonjwa mbali mbali kama vile kisukari,presha,magonjwa ya moyo n.k, Pia mazoezi huweza kuwa tiba, mfano; kwa mama aliyefanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua,mazoezi huweza kusaidia kidonda chake kupona kwa haraka zaidi.” image-1=”” count=”2″ html=”true” css_class=””]

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.