Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Parkinson’s ni ugonjwa gani,vihatarishi vyake

Parkinson’s ni ugonjwa gani,vihatarishi vyake;

Parkinson’s ni Ugonjwa gani

Parkinson’s ni ugonjwa ambao kwa kiasi kikubwa unaathiri mfumo wa neva, na ambao husababisha seli za neva (neurons) katika eneo la ubongo kudhoofika na kufa.

Huu ni ugonjwa ambao huhusisha ubongo wa binadamu kushindwa kufanya kazi vizuri kutokana na ukosefu wa vichocheo aina ya Dopamini.

Fahamu kwamba,Seli za nerves au Neuron huzalisha kemikali inayoitwa dopamine, ambayo ubongo unaihitaji kwa kiasi fulani ili kudhibiti mwendo yaani movements kwa Mtu,

Neurons zikiwa dhaifu huzalisha viwango vya chini vya dopamine,

Ingawa kwa asilimia kubwa chanzo cha neurons hizi kudhoofika hakijulikani bado.

Baadhi ya wagonjwa walio na ugonjwa wa Parkinson pia wanakabiliwa na tatizo la kupungua kwa norepinephrine,

kemikali ambayo huweza kusaidia kudhibiti kazi mbalimbali mwilini, kama vile udhibiti wa shinikizo la damu pamoja na mapigo ya moyo.

Kwa Mujibu wa Parkinson’s Foundation; Zaidi ya watu milioni 10 duniani kote kwa sasa wanaishi na ugonjwa wa Parkinson.

SABABU ZINAZOONGEZA
HATARI YA MTU KUPATA UGONJWA HUU WA PARKINSON

1. Jinsia; Wanaume wana uwezekano wa kuwa na Ugonjwa huu mara 1.5 zaidi kuliko wanawake.

2. Umri; Hatari ya Ugonjwa wa Parkinson huongezeka kadiri umri unavyoongezeka,

ingawa watu wengine hugunduliwa Ugonjwa huu mapema kabla ya umri wa miaka 50.

3. Jenetiki; Uwepo wa genes za tatizo hili katika Familia yako, huweza kuongeza hatari ya wewe kupata ugonjwa huu wa Parkinson,

4. Sababu za Kimazingira;Uchunguzi umeonyesha uhusiano kati ya kuathiriwa na kemikali zinazotumiwa katika viuatilifu na viua magugu,metals mbali mbali na vichafuzi yaani-organic pollutants na ugonjwa wa huu wa Parkinson.

5. Kuumia eneo la kichwani,Pia Kupigwa mara kwa mara au Kuumia eneo la kichwani kunaweza kuongeza hatari ya mtu kupata Ugonjwa huu wa Parkinson, N.k

Ingawa sio kila anaeumia Eneo la kichwani basi lazima apate ugonjwa huu wa parkinson.

DALILI ZA UGONJWA WA PARKINSON

Dalili za ugonjwa wa Parkinson mara nyingi huanza hatua kwa hatua na kuendelea kwa muda:

Na baadhi ya Dalili hizo ni Pamoja na;

  •  Mtu Kutetemeka
  • Misuli kukakamaa na kuwa migumu
  •  Kupata Ugumu wa kutembea
  • Usawa usio thabiti
  •  Kuwa na shida ya Poor posture
  • Kupungua kwa harakati mbali mbali za mwili (bradykinesia)

DALILI ZA UGONJWA WA PARKINSON

Je mtu mwenye Ugonjwa wa Parkinson utamjuaje?. Dalili kubwa za Ugonjwa wa Parkinson ni pamoja na;

  1.  Kuwa na hali ya kutetemeka Mikono
  2.  Kazi za ubongo kuathiriwa kama uwezo wa kutunza kumbu kumbu kupotea
  3.  Uwezo wa kufikiria kuathirika
  4. Mgonjwa kupata shida ya kushindwa kutembea
  5. Mgonjwa kujaa hofu na wasiwasi kwa muda mwingi
  6.  Mgonjwa kuwa na hali ya huzuni kwa kiasi kikubwa katika maisha yake
  7. Mgonjwa kupata tatizo la kukosa Usingizi
  8. Mgonjwa kuwa hali ya mahangaiko au kutokutulia kila mara

WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;

✓ Walio katika ukoo ambao kuna mtu mwenye shida hii,kwani huaminika kwamba vinasaba vya ugonjwa huu hurithiwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine.

✓ Wanaofanya kazi ambazo huhusisha kwa kiasi kikubwa upuliziaji wa makemikali katika mimea.

✓ Ugonjwa huu wa Parkinson hupata Wanaume zaidi ya Wanawake.

MATIBABU YA UGONJWA WA PARKINSON

Hakuna Matibabu ya moja kwa moja ya ugonjwa wa Parkinson  mpaka sasa.Ila kuna matibabu yakudhibiti Dalili za Ugonjwa huu kama vile;

Matumizi ya Dawa kama Sinemet pamoja na Levodopa ambazo huhusika na kuzuia hali ya kutetemeka kwa mgonjwa,hofu,wasiwasi, pamoja na shida ya kushindwa kulala.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.