Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Sababu za Uti Sugu: Kuzuia na Kutibu Hali Hii

Sababu za Uti Sugu: Kuzuia na Kutibu Hali Hii

UTI Sugu(Chronic urinary tract infections) ni maambukizi ya bacteria kwenye njia ya mkojo ambayo hutokea kwa kujirudia rudia,endelevu au ambayo hayaponi licha ya kupata Tiba. 

Maambukizi haya huweza kuhusisha njia ya mkojo,Kibofu cha Mkojo,Figo n.k

Dalili za UTI Sugu ni Pamoja na;

  1. Mtu kukojoa mara kwa mara
  2. Kukojoa mkojo mweusi au kukojoa damu(bloody or dark urine)
  3. Kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa
  4. Kupata maumivu kwenye eneo la Figo,hasa upande wa chini kidogo ya mbavu au nyuma ya mgongo
  5. Kupata maumivu kwenye eneo la kibofu cha Mkojo

Na endapo UTI itasambaa mpaka kwenye Figo,basi mgonjwa huweza kupata dalili hizi;

  • Kuhisi hali ya kichefuchefu na kutapika
  • Joto la mwili kuwa juu(38°C) au mgonjwa kuwa na homa
  • Mwili kutetemeka
  • Mwili kuchoka kupita kiasi
  • Kupata dalili zote za matatizo ya akili(mental disorientation) n.k
  • Maumivu makali ya Uti wa mgongo

Kwa wengi wetu, maumivu ya uti wa mgongo ni suala la kawaida, lakini kwa wengine, hali hii inaweza kuwa kubwa sana na kuathiri maisha yao ya kila siku,

Hii ni kwa sababu ya UTI sugu, hali ambayo husababisha maumivu ya uti wa mgongo kwa zaidi ya wiki 12. Hali hii inaweza kuathiri mtu yeyote, lakini ni kawaida zaidi kwa watu wenye umri wa kati ya miaka 30 hadi 50.

Mashambulizi ya bacteria hawa yanaweza kufika mpaka kwenye kibofu cha Mkojo,Na Tafiti zinaonyesha bacteria E. coli ndyo aina ya bacteria ambao hushambulia sana eneo la kibofu cha mkojo,

Kwa bahati mbaya, sababu za uti kuwa sugu hazijulikani wazi, lakini kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kuathiri na kuongeza hatari ya mtu kuwa nayo.

Katika makala hii, tutaangalia sababu za uti sugu, jinsi ya kuzuia hali hii, na jinsi ya kutibu ikiwa inaendelea.

Sababu za Uti Sugu

Sababu hizi huongeza hatari ya mtu kupata UTI sugu,Sababu za maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) ya muda mrefu ni pamoja na:

  1. Kukaa na mkojo kwa muda mrefu kwenye kibofu cha mkojo.
  2. Kufanya mapenzi mara kwa mara bila kutumia Kinga na mtu mwenye maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama vile bacteria
  3. Kuwa na kisukari au magonjwa mengine ambayo huweza kudhoofisha kinga yako ya Mwili.
  4. Kutumia dawa mbali mbali  za kupaka kwenye uke au uume wakati wa kufanya mapenzi zinaweza kusababisha maambukizi pia
  5. Kuwa na tatizo la kibofu cha mkojo au upasuaji wa awali wa kibofu cha mkojo.

Kuna sababu kadhaa ambazo zinaweza kuongeza hatari ya mtu kuwa na uti sugu. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na:

1. Umri: Kama tulivyosema hapo awali, watu kati ya miaka 30 na 50 wana hatari kubwa zaidi ya kuwa na uti sugu.

2. Jinsia: Wanawake wana hatari kubwa zaidi ya kuwa na uti sugu kuliko wanaume.

3. Mabadiliko ya vichocheo mwilini(hormones change) ambayo huweza kuathiri hali ya bacteria Ukeni,

Hii hutokea hasa kwa wanawake wanaofika Ukomo wa hedhi yaani menopause.

4. Kazi: Aina ya Kazi unayofanya inaweza kuongeza hatari ya kuwa na uti sugu. Mfano kazi za kukaa kwenye mazingira ya maji maji sana n.k

5. Kutumia vyoo vinavyotumiwa na watu wengi zaidi(Public toilets),

unaweza kuwa kwenye hatari ya kupata UTI Sugu ikiwa unatumia vyoo vinavyotumiwa na watu wengi hasa vikiwa havifanyiwi Usafi Vizuri.

6. Historia ya familia: Ikiwa mtu ana mwanafamilia aliye na uti sugu, ana hatari kubwa ya kuwa nayo pia.

7. Kutumia vifaa kama Sex Toys, Baadhi ya sabuni zenye kemikali,mafuta n.k huweza kuharibu mazingira ya Ukeni na kupelekea maambukizi zaidi ya bacteria Ukeni.

8. Pamoja na Hali ya Usafi binafsi,

Jinsi ya Kuzuia Uti Sugu

Kuzuia uti sugu ni bora kuliko kutibu. Kuna hatua kadhaa ambazo mtu anaweza kuchukua ili kuzuia uti sugu. Hatua hizo ni pamoja na:

✓ Zingatia Usafi, Hakikisha usafi wa Mazingira kama vyoo,Maji ujayotumia toilets, Pamoja na usafi wako binafsi

✓ Kufanya mazoezi mara kwa mara:

Mazoezi ya mara kwa mara husaidia kuimarisha Kinga ya Mwili na kusaidia kuepuka mashambukizi ya vimelea kama bacteria kwa urahisi zaidi

✓ Epuka matumizi ya Sabuni,mafuta n.k yenye kemikali ambazo huweza kuathiri mazingira ya Ukeni

✓ Hakikisha unakunywa Maji mengi kila siku, kunywa angalau glass 8 au lita 2.5 mpaka 3 kwa Siku,

Ingawa kiwango cha maji unayokunywa huweza kutegemea na umri wako,Uzito,kazi unayofanya,mazoezi,hali ya mazingira,afya yako kwa ujumla n.k

✓ Kula Mlo wenye Virutubisho vyote Muhimu, kama vile Proteins,vitamins,madini n.k

FAQs

[sc_fs_multi_faq headline-0=”h3″ question-0=”Ni nini Maana ya uti sugu?” answer-0=”UTI Sugu(Chronic urinary tract infections) ni maambukizi ya bacteria kwenye njia ya mkojo ambayo hutokea kwa kujirudia rudia,endelevu au ambayo hayaponi licha ya kupata Tiba. ” image-0=”” headline-1=”h3″ question-1=”Zipi ni dalili za uti sugu?” answer-1=”Dalili za UTI Sugu ni pamoja na mtu kukojoa mara kwa mara,Kukojoa mkojo mweusi au kama damu(bloody or dark urine),Kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa n.k” image-1=”” count=”2″ html=”true” css_class=””]

Hitimisho

Uti sugu ni tatizo ambalo huwapata watu wengi hasa wanawake, Tatizo hili linaweza kusababisha maumivu makali ya mgongo,mtu kukojoa mkojo mweusi au kama damu,kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa,Homa,uchovu,maumivu makali ya tumbo n.k.

Kuzuia uti sugu ni muhimu zaidi kuliko kutibu, na kuna hatua kadhaa ambazo mtu anaweza kuchukua ili kuzuia tatizo hili kama tulivyokwisha kueleza hapo Juu.

Ikiwa mtu tayari ana uti sugu, kuna hatua kadhaa ambazo anaweza kuchukua ili Kutibu na kuzuia madhara zaidi.

Ni muhimu kutambua dalili za uti sugu mapema ili kuchukua hatua na kuzuia tatizo hili kusababisha shida kubwa zaidi.

Endapo unapata Dalili kama nilizozitaja hapa,Hakikisha unaenda Kufanya vipimo.

SOMA Zaidi:Dalili za UTI Sugu kwa Mwanamke na Mwanaume.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.