Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la lowsperm count kwa mwanaume ni nini

Tatizo la lowsperm count kwa mwanaume ni nini

Baadhi ya Wanaume wanasema ni tatizo la shahawa kuwa nyepesi, je hi ni sahihi? Soma zaidi hapa Kujua

Low sperm count ni tatizo ambalo huhusisha uwepo wa kiwango kidogo cha Mbegu za Kiume kuliko kawaida kwa kila bao unalopiga,

[sc_fs_faq html=”true” headline=”h3″ img=”” question=”Lowsperm count ni nini?” img_alt=”” css_class=””] Low sperm count ni tatizo ambalo huhusisha uwepo wa kiwango kidogo cha Mbegu za Kiume kuliko kawaida kwa kila bao unalopiga, [/sc_fs_faq]

Kwa jina lingine tatizo la low sperm count hujulikana kama oligospermia,

Kumbuka, Tofautisha Lowsperm count na tatizo la azoospermia, ambapo Azoospermia huhusisha mwanaume kutokuwa na mbegu za Kiume kabsa.

Je ni wakati gani tunaweza Kusema Mwanaume ana kiwango kidogo cha Mbegu za kiume?

Ni Pale ambapo ana kiwango cha chini ya Mbegu million 15 kwa Milliliter za Semen( fewer than 15 million sperm per milliliter of semen).

DALILI ZA TATIZO LA LOWSPERM COUNT

– Mojawapo ya dalili kubwa ni Mwanaume kutokuwa na uwezo wa Kutungisha Mimba,

Ishara kuu ya idadi ndogo ya manii ni kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto,

Huenda kusiwe na dalili zingine ambazo zinaonekana kwako, Lakini kupitia hii,ikakupa Mwanga wa kufanya Vipimo kujua shida ni nini,

Ingawa sio kila Mwanaume mwenye shida ya kushindwa kumpa Mwanamke Mimba,basi ana tatizo la Lowsperm count,

Huenda kukawa na matatizo mengine kama vile; Tatizo la hormone imbalance, Mirija ya Kupitisha mbegu za kiume(Sperm ducts) kuziba n.k

– Pia tatizo hili la Lowsperm count huweza kuambatana na dalili zingine kama vile;

  • Uume kushindwa kusimama vizuri,Upungufu wa nguvu za kiume
  •  mwanaume kukosa hamu ya kufanya mapenzi
  •  Maumivu au uvimbe kwenye eneo la korodani
  • Kupungua kwa nywele za usoni au mwilini au ishara zingine za upungufu wa homoni n.k

Ni Wakati Gani wa kuonana na daktari?

Muone daktari ikiwa hujaweza kupata mtoto baada ya mwaka mzima wa kutafuta mtoto bila mafanikio,

au hata kabla ya Mwaka,Muone daktari mapema zaidi ikiwa una mojawapo ya yafuatayo:

1. Matatizo ya Uume kushindwa kusimama au kumwaga manii,

2. Kuwa na hamu ndogo ya kufanya tendo la ndoa au kutokuwa na hamu kabsa ya tendo la ndoa

3. Kupata Maumivu au uvimbe kwenye eneo la korodani

4. Kuwa na Historia ya tezi dume

5. kuumwa magonjwa ya Zinaa(STIs)

6. Kuwa na historia ya Upasuaji wa groins, uume au korodani

CHANZO CHA TATIZO LA LOWSPERM COUNT

Ingawa inaweza kuwa Vigumu kugundua Sababu ya Moja kwa moja ambayo inasababisha tatizo la lowsperm count,

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu ambazo huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili la Lowsperm count kwa kiwango kikubwa;

– Matatizo kwenye hormones

– Mbegu za kiume kutokuwa na umbo linalotakiwa yaani abnormal sperm shape (morphology)

– Tatizo la kuvimba kwa Mshipa wa vein yaani Varicocele

– Maambukizi ya magonjwa mbali mbali hasa yale ambayo huweza kuathiri uzalishwaji wa mbegu za kiume,kuziba kwa mrija wa kupitisha mbegu za kiume,au Kusababisha uvimbe kwenye maeneo kama vile Korodani pamoja na epididymis,

Mfano;maambukizi ya magonjwa ya Zinaa kama vile Kisonono pamoja na Virusi vya Ukimwi.

– Kuwa na tatizo la Retrograde ejaculation ambapo mbegu za kiume huingia kwenye kibofu cha Mkojo badala ya kutoka nje wakati wa tendo la ndoa,

Hii huweza kusababisha na matatizo mbali mbali kama vile,Ugonjwa wa kisukari,Kuumia eneo la Uti wa mgongo(Spinal injuries), kufanyiwa upasuaji kwenye kibofu cha Mkojo,Tezi dume au eneo la urethra.

– Matumizi ya baadhi ya Dawa

– Kuwa na Tatizo la Uvimbe

– Kuwa na tatizo la Korodani kutokushuka chini kama kawaida yaani Undescended testicles,

Fahamu kwamba,baada ya Mtoto wa Kiume kuzaliwa anatakiwa korodani zake ziwe zimeshuka chini tayari kwenye kifuko chake yaani SCROTUM,

Ila wakati mwingine,Kipindi cha ukuaji wa mtoto tumboni,Korodani moja au zote mbili zinashindwa kushuka chini kutoka tumboni na kuingia kwenye kifuko chake(Scrotum) kama kawaida,

Tatizo hili huathiri kwa kiwango kikubwa Uzalishwaji wa mbegu za kiume na hata kupelekea mwanaume kushindwa kumpa mwanamke Mimba.

– Kuwa na tatizo la Kuziba Mrija wa Kusafirisha mbegu za kiume(Sperm ducts)

– Kuwa na matatizo ya kwenye vinasaba(Chromosome defects).

Hapa nazungumzia matatizo kama vile Klinefelter’s syndrome, ambapo mwanaume huzaliwa akiwa na chromosomes “X” mbili na “Y” moja badala ya kuwa na “X” moja na “Y” moja

MBEGU ZA KIUME

XXY= hii sio kawaida

XY= hii ni kawaida

– kuwa kwenye mazingira yenye kemikali, Heavy metals, mionzi ya X-rays n.k

– Korodani Kupata joto kupita kiasi, kwasababu mbali mbali,

ikiwemo kuvaa nguo za ndani za kubana sana, zenye material ya Mpira,kukaa kwa muda mrefu sana n.k

– Matumizi ya dawa za Kulevyia kama vile cocaine au marijuana

– Uvutaji wa Sigara,Tumbaku n.k

– Matumizi ya Pombe Kupita Kiasi, Fahamu Pombe huweza kupunguza kiwango cha hormones aina ya testosterone hali ambayo huweza kupelekea kupungua kwa uzalishwaji wa mbegu za kiume

– Msongo mkali wa Mawazo,watu wengi hawafahamu kwamba msongo wa mawazo huweza kuathiri uwezo wa tendo kwa mwanaume,na hata kusababisha kupungua sana kwa Uzalishwaji wa mbegu za kiume

– Tatizo la Uzito Mkubwa na Unene(Overweight/Obesity) n.k

VITU HIVI HUONGEZA HATARI ZAIDI YA WEWE KUPATA TATIZO LA LOWSPERM COUNT

  1.  Unywaji wa Pombe
  2. Uvutaji wa Tumbaku
  3. Kutumia dawa za Kulevyia kama Cocaine,marijuana n.k
  4. Kuwa na Uzito mkubwa kupita kiasi
  5. Kuwa na Msongo mkali wa Mawazo
  6. Kuwa na maambukizi ya magonjwa ambayo hayaishi
  7.  Kuumia eneo la Korodani
  8. Korodani zako Kupata Joto Kupita kiasi
  9. Kuwa kwenye mazingira ya kemikali au Mionzi n.k
  10.  Kuwa na tatizo la Uvimbe kwenye Korodani n.k

FANYA HAYA ILI KUJIKINGA

✓ Epuka uvutaji wa Sigara au tumbaku

✓ Acha kabsa au dhibiti sana Matumizi ya Pombe

✓ Epuka matumizi ya dawa za kulevyia kama vile cocaine au marijuana

✓ Dhibiti Uzito wako wa Mwili na kuepuka tatizo la Uzito mkubwa

✓ Dhibiti Msongo wa Mawazo

✓ Epuka matumizi ya dawa pasipo na maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya

✓ Dhibiti hali yoyote inayopelekea korodani zako kupata JOTO kupita kiasi n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.