Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dalili za ugonjwa wa covid 19,Chanzo na Matibabu yake

Dalili za ugonjwa wa covid 19,Chanzo na Matibabu yake

 UGONJWA WA COVID19 NI NINI?

Huu ni ugonjwa wa kuambukiza ambao umesababishwa na kirusi aina mpya cha corona, Ugonjwa huu wa covid 19 ulianzia jiji la Wuhan, nchini China mwezi Disemba 2019.

JE UGONJWA WA COVID19 UNASAMBAA VIPI?

Ugonjwa wa covid 19 huweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mtu mwingine kupitia vitone vidogo vidogo vya mate vinavyoruka toka puani au mdomoni pale mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Corona anapopiga chafya , kukohoa au kupumua.

Vitone hivi vya mate huweza kutua kwenye nyuso za watu au vitu, watu wengine hupata virusi hivi wanapogusa hivi vitu,

Vitone hivi vikiruka hewani mtu anapopiga chafya au kukohoa mtu mwingine huweza kuvivuta ndani na hewa anapopumua, hivyo ni muhimu kukaa umbali wa mita 1 kutoka kwa mtu anayeumwa ili kujikinga na ugonjwa wa covid 19.

DALILI ZA UGONJWA WA COVID19 NI ZIPI?

Dalili za ugonjwa wa COVID19 kwa wagonjwa wengi ni pamoja na;

  • homa,
  • uchovu
  • Pamoja na kikohozi kikavu.

Wagonjwa wengine hupata dalili kama;

  • misuli kuuma,
  • pua kubana,
  • mafua kutiririka,
  • maumivu ya koo
  • au kuharisha.

Dalili hizi huwa ni ndogo na huanza taratibu.

Endelea Zaidi hapa kusoma Dalili za ugonjwa wa covid 19,

DALILI ZA ugonjwa wa covid 19,

1. Mgonjwa, joto la mwili kupanda au kupata homa

2. Mgonjwa kupata maumivu makali ya kifua wakati wa kukohoa

3. Mgonjwa kubanwa na mbavu

4. Mgonjwa kupatwa na Mafua makali yanayoambatana na kichwa kuuma sana

5. Mgonjwa kupata Kikohozi kikavu

6. Mgonjwa kupata uchovu wa mwili kupita kiasi

7. Mgonjwa kushindwa kupumua au kupata shida wakati wa kupumua

8. Mgonjwa kupoteza hamu ya kula

9. Wakati mwingine Mgonjwa kuharisha( Nadra) n.k

UCHUNGUZI WA ugonjwa wa covid 19,

Moja ya vitu ambavyo huchunguzwa ni pamoja na joto la Mwili, mate au sampuli za Damu za mtu ambaye anaonyesha dalili hizi za ugonjwa wa covid 19.

NJIA ZA KUJIKINGA NA ugonjwa wa covid 19,

1. Nawa vizuri mikono yako kwa sabuni na maji safi

2. Epuka kukaa maeneo yenye Msongamano wa watu wengi

3. Funika mdomo wako kwa kutumia masks au maarufu kama Barakoa

4. Epuka kuwa karibu au kugusana na mtu mwenye dalili

5. Epuka kusalimia watu kwa kuwashika Mikono

JE UNAWEZA VIPI KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA COVID19

– Nawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia dawa maalumu ya kuua wadudu (Hand sanitizer)

Kwa nini? Ukinawa mikono kwa sabuni na maji au kutumia dawa maalumu ya kusafisha mikono utaondoa virusi ambao hukaa kwenye mikono mara nyingi,

Hii ni moja ya Njia muhimu sana ya kujikinga na ugonjwa wa covid 19.

– Jiweke mbali zaidi ya mita moja kutoka kwa mtu anayekohoa au kupiga chafya,

Kwa nini? Mtu anapopiga chafya au kukohoa hurusha vitone au chembechembe za mate ambazo huweza kuwa zimebeba virusi. Ukiwa karibu sana utawavuta virusi hawa unapovuta hewa kupumua.

– Acha kushikashika macho, pua na mdomo kwa mikono ambayo hujaisafisha

Kwa nini? Mikono hugusa sehemu mbalimbali hivyo huweza kubeba virusi. Unapogusa macho ,pua au mdomo virusi hupata njia ya kuingia mwilini na kukufanya upate ugonjwa wa covid 19.

– Iwapo unaumwa mafua, homa au shida ya kupumua usiendelee na shughuri zako nenda hospitali

Kwa nini? Vituo vya huduma ya afya vina taaarifa zote kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa covid 19 pia huweza kukupatia tiba sahihi kuhusu tatizo lako pia hukulinda na kusaidia usisambaze maambukizi kwa watu wengine.

– Kutokushikana mikono au kukumbatiana, hii pia ni mojawapo ya njia za kukukinga dhidi ya ugonjwa wa covid 19.

FAQs: Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, kuepuka kushikana mikono inaweza kusaidia kukukinga na ugonjwa wa covid 19,

Ndyo, Moja ya Njia ya kukukinga na ugonjwa wa covid 19, ni pamoja na kuepuka kushikana mikono.

Hitimisho

Ugonjwa wa covid 19, ni miongoni mwa magonjwa ya mlipuko ambayo yamesababisha Vifo Vingi Zaidi duniani,

Unaweza kujikinga na ugonjwa wa covid 19 kwa kutumia Njia hizi;Hakikisha unapata chanjo ya Kuzuia ugonjwa wa covid 19,Nawa mikono kila mara kwa maji Safi tiririka pamoja na sabuni,

Epuka kukaa maeneo yenye Msongamano wa watu wengi,Funika mdomo wako kwa kutumia masks au maarufu kama Barakoa hasa unapokuwa sehemu za watu wengi, Epuka kuwa karibu au kugusana na mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Covid 19,Epuka kusalimia watu kwa kuwashika Mikono n.k

Ukiona dalili Zozote ambazo huzielewi hakikisha unawahi hospital kwa ajili ya uchunguzi Zaidi,

Kwa Kuzingatia njia hizi unaweza kujikinga na Ugonjwa wa Covid 19.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.