Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Lishe Bora kwa Wajawazito Walio na Matatizo ya Kiafya Tanzania

Lishe Bora kwa Wajawazito Walio na Matatizo ya Kiafya Tanzania

Kuwa na ujauzito ni hatua kubwa katika maisha ya mwanamke,Wakati huo huo, inaweza kuwa changamoto kubwa kwa wale ambao wana matatizo ya kiafya kama kisukari, shinikizo la damu, au unene kupita kiasi.

Hata hivyo, kwa kufuata lishe bora, wajawazito wanaweza kuwa na afya nzuri na kuepuka matatizo ya kiafya kwa mama na mtoto,Makala hii inajadili lishe bora kwa wajawazito walio na matatizo ya kiafya nchini Tanzania.

Vyakula hivi ni Faida kwa Afya ya Mama Mjamzito pamoja na Mtoto aliyetumboni kwa Ujumla(Hapa hatunzumzii wenye matatizo ya kiafya kama presha,kisukari,magonjwa ya moyo n.k)

✓ Kula Mboga za Majani na viungio vyake,mfano:

  • spinach,
  • Mchicha
  • Tembele
  • karoti,
  • viazi vitamu
  • nyanya na pilipili tamu nyekundu (kwa vitamini A na potasiamu)

✓ Kula Matunda mbali mbali kama vile;

  • tikitimaji,
  • maembe,
  • ndizi,
  • parachichi,
  • machungwa,
  • Pamoja na zabibu nyekundu au pink (kwa potasiamu)

✓ Maziwa: maziwa fresh au mtindi usio na mafuta kabsa au mafuta kidogo,maziwa ya soya(kwa ajili ya kupata kalsiamu, potasiamu, vitamini A na D)

✓ Nafaka: nafaka zilizo tayari kuliwa/nafaka zilizopikwa (kwa ajili ya madini chuma na foliki asidi)

✓ vyakula vyenye virutubisho vya Protini kama vile:

  • maharagwe na mbaazi;
  • karanga na mbegu;
  • nyama ya ng’ombe, kondoo,
  • Samaki n.k;

Lishe Bora kwa Wajawazito Walio na Matatizo ya Kiafya Tanzania

Chini ni orodha ya lishe bora kwa wajawazito walio na matatizo ya kiafya nchini Tanzania:

1. Chagua chakula chenye virutubisho muhimu

Wajawazito walio na matatizo ya kiafya wanapaswa kuchagua chakula chenye virutubisho muhimu kama;

  • protini,
  • wanga,
  • mafuta yenye afya,
  • madini
  • Pamoja na vitamini.

Protini husaidia katika ukuaji wa seli za mtoto na kiwango cha hemoglobini kwenye damu ya mama.

Wanga hupatikana katika;

  • mchele,
  • ngano,
  • viazi,
  • mahindi na ndizi.

Mafuta yenye afya yanaweza kupatikana katika;

  • samaki,
  • karanga,
  • na mafuta ya mzeituni.

Madini na vitamini vinapatikana katika;

  • matunda,
  • mboga mboga,
  • na vyakula vingine vya kijani.

2. Kula mara nyingi kidogo kidogo

Wajawazito wanapaswa kula mara nyingi kidogo kidogo badala ya kula kwa wingi mara moja. Hii husaidia kuzuia kushuka kwa sukari kwenye damu na kudumisha kiwango cha sukari cha kawaida. Pia inasaidia katika kuzuia tumbo kujaa gesi,kiungulia n.k

3. Epuka vyakula vyenye sukari nyingi

Wajawazito walio na matatizo ya kiafya wanapaswa kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi kama vile pipi, biskuti, na vinywaji vyenye sukari.

Vyakula hivi vinaweza kusababisha ongezeko la sukari kwenye damu na kuathiri hali ya kiafya ya mama na mtoto

4. Punguza ulaji wa chumvi

Wajawazito walio na matatizo ya kiafya wanapaswa kupunguza ulaji wa chumvi,

Kula chakula chenye kiwango kidogo cha chumvi kunasaidia katika kudhibiti shinikizo la damu na kuzuia matatizo mengine kama vile kuvimba kwa mwili ikiwemo miguu n.k

5. Kunywa maji mengi

Wajawazito wanapaswa kunywa maji mengi ili kuhakikisha mwili wao unakuwa na maji ya kutosha.

Maji husaidia katika kuzuia kuvimba kwa mwili na husaidia katika kusafisha figo.

6. Kula vyakula vyenye Virutubisho muhimu

Wajawazito wanapaswa kula vyakula vyenye Virutubisho muhimu kwa mama na Mtoto,

Kula mlo wenye afya kama vile matunda, mboga mboga, nafaka zisizokobolewa, vyakula vyenye protini kama vile samaki, kuku, na maharage.

Hii inasaidia katika kudumisha afya na kuepuka matatizo ya kiafya.

7. Epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi

Wajawazito wanapaswa kuepuka kula kwa wingi vyakula vyenye mafuta mengi kama vile;

  • nyama nyekundu,
  • viazi(chips),
  • Pamoja na nyama ya kukaanga.

Kula vyakula hivi kunaweza kuongeza hatari ya kupata kisukari na matatizo mengine ya kiafya.

FAQs

Je, ni lishe gani nzuri kwa wajawazito walio na matatizo ya kisukari?

Wajawazito walio na matatizo ya kisukari wanapaswa kula chakula chenye kiwango cha sukari cha chini na kupunguza ulaji wa wanga. Pia wanapaswa kula vyakula vyenye mafuta yenye afya na kufanya mazoezi ya kutosha.

Je, ni vyakula vipi vinavyopaswa kuepukwa na wajawazito walio na shinikizo la damu?

Wajawazito walio na shinikizo la damu wanapaswa kuepuka kula vyakula vyenye kiwango cha juu cha chumvi, vyakula vyenye sukari nyingi, na vyakula vyenye mafuta mengi.

Hitimisho(Conclusion)

Kama ilivyoelezwa hapo juu, ni muhimu kwa wajawazito walio na matatizo ya kiafya kuhakikisha kuwa wanakula lishe bora,

Kula vyakula chenye virutubisho muhimu, kunywa maji mengi, kula mara nyingi kidogo kidogo, na kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta mengi ni muhimu katika kudumisha afya ya mama na mtoto.

Kwa kuwa na lishe bora, wajawazito wanaweza kuepuka matatizo ya kiafya na kufurahia ujauzito wao kwa amani na utulivu.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.