Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Njia za kupunguza hatari ya kupata saratani, Jikinge na Saratani mbali mbali

Njia za kupunguza hatari ya kupata saratani, Jikinge na Saratani mbali mbali

Moja ya Magonjwa ambayo husababisha vifo vingi ni Pamoja na Saratani, Zipo Saratani za aina mbali mbali kama vile; Saratani ya matiti,Saratani ya mlango wa kizazi,Saratani ya Mapafu n.k

Katika Makala hii tutachambua kuhusu Njia za kupunguza hatari ya kupata saratani mbali mbali,

Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO);

Hizi hapa Chini ni baadhi Saratani ziliongoza kuwapata Watu wengi zaidi ndani ya Mwaka 2020;

  1. Saratani ya Matiti-breast cancer(2.26 million cases);
  2. Saratani ya Mapafu-lung cancer(2.21 million cases);
  3. Saratani ya Utumbo mpana yaani colon cancer pamoja na rectum cancer (1.93 million cases);
  4. Saratani ya Tezi Dume-prostate cancer (1.41 million cases);
  5. Saratani ya ngozi-skin cancer (non-melanoma) (1.20 million cases); and
  6. Na Saratani ya tumbo-stomach cancer (1.09 million cases).

Njia za kupunguza hatari ya kupata saratani

Unaweza kupunguza hatari ya Kupata Saratani za aina mbali mbali kwa kufanya na kuzingatia baadhi ya mambo haya;

1. Kwanza Fanya Vipimo yaani Screening tests mara kwa mara ili kugundua Saratani hata zikiwa kwenye hatua za mwanzoni,

Kumbuka; Saratani yoyote inaweza kutibika haraka endapo ikigundulika mapema na kupata matibabu sahihi kwa wakati, madhara Zaidi hutokea na hata Vifo ukichelewa Zaidi kupata Matibabu.

2. Pata Chanjo,

Moja ya Njia za kupunguza hatari ya kupata saratani ni Pamoja na Kupata Chanjo kwa aina za saratani ambazo zina chanjo ya Kuzuia watu kupata,

Mfano kama Saratani ya Mlango wa Kizazi ambayo kwa asilimia kubwa husababishwa na Virus vya human papilloma Virus(HPV), hii ina chanjo na chanjo yake tayari inatolewa kwa watu mbali mbali.

3. Epuka Uvutaji wa Sigara na Tumbaku(tobacco)

Moja ya Njia za kupunguza hatari ya kupata saratani mbali mbali ni pamoja na kuacha kabsa Uvutaji wa Sigara

Saratani kama vile;

  • Saratani ya MAPAFU(Lung cancer)
  • Saratani ya Koo n.k

huweza kusababishwa kwa kiwango kikubwa na uvutaji wa Sigara

4. Hakikisha unadhibiti tatizo la Uzito Mkubwa

Watu wenye Uzito Mkubwa au wanene wanaongeza hatari ya kupata Saratani mbali mbali, hivo kudhibiti Uzito ni mojawapo ya Njia za kupunguza hatari ya kupata saratani

5. Epuka matumizi ya Pombe Kupita kiasi

6. Linda ngozi yako kwa njia mbali mbali

kulinda ngozi yako dhidi ya kemikali hatari,mionzi ya jua na mionzi mingine ni Njia mojawapo ya kupunguza hatari ya kupata saratani ya Ngozi.

7. Kula Lishe bora,bila kusahau matunda pamoja na mboga za majani

Hapa utapata antioxidants ambazo zitasaidia kupunguza hatari ya Kupata Saratani mbali mbali.

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je Kuna Njia za kupunguza hatari ya kupata saratani?

Ndyo,Njia za kupunguza hatari ya kupata saratani ni pamoja na kupata chanjo, kula lishe bora,kufanya mazoezi,kujikinga na mionzi mikali,kuepuka matumizi ya pombe kupita kiasi,kuepuka uvutaji wa Sigara pamoja na tumbaku.

Hitimisho;

Saratani ni tatizo ambalo husababisha Vifo vingi Duniani bila kujali umri wala jinsia, lakini unaweza kupata Tiba na kupona kabsa endapo imegundulika mapema,hivo jenga tabia ya kufanya Vipimo Mara kwa mara.

Kwa bahati Nzuri,zipo Njia za kupunguza hatari ya kupata saratani mbali mbali,

Tumia njia hizi kupunguza hatari ya Kupata Saratani mbali mbali;pata chanjo, kula lishe bora,fanya mazoezi,jikinge na mionzi mikali,epuka matumizi ya pombe kupita kiasi,epuka uvutaji wa Sigara pamoja na tumbaku, Pia hakikisha unadhibiti Uzito wako wa mwili ili kuepuka tatizo la Uzito mkubwa(Overweight/obesity).

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.