Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu (Vasculitis),chanzo,dalili na Tiba

Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu (Vasculitis),chanzo,dalili na Tiba

Vasculitis ni Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu, kuna aina mbali mbali za ugonjwa huu wa kuvimba kwa mishipa ya damu ingawa aina nyingi ni adimu kutokea.

Katika Makala hii tunachambua zaidi kuhusu Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu (Vasculitis),chanzo,dalili na Tiba yake.

Dalili za Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu

Bila kuangalia aina moja moja,kwa Ujumla dalili za Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu ni pamoja na;

– mgonjwa Kupata homa

– Kupata maumivu ya kichwa

– Uzito wa mwili kupungua

– Kupata maumivu ya viungo,joints,misuli pamoja na mwili kwa ujumla

– Kama Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu umeathiri tumbo au utumbo, basi utapata maumivu baada ya kula chakula

– Kusababisha macho kuwa mekundu pamoja na kuwasha au kuhisi hali ya kuungua

– Baadhi ya aina za Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu(vasculitis) huweza kusababisha miguu kuchoma choma au kuwa dhaifu zaidi,

pia eneo la chini ya miguu pamoja na viganja vya mikono vinaweza kuvimba au kuwa vigumu zaidi.

– Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu unaweza kusababisha mtu kukosa pumzi au hata kukohoa damu kama umeathiri eneo la mapafu.

– Pia Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu unaweza kusababisha damu kuvuja chini ya ngozi kisha kupelekea madoa mekundu kuonekana kwenye ngozi(tazama mfano kwenye picha)

Chanzo cha Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu

Sababu halisi inayosababisha Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu bado haifahamiki, ingawa kuna baadhi ya Sababu zimeonekana kuwa na uhusiano wa karibu sana na Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu, sababu hizo ni pamoja na;

– Swala la vinasaba,genes au genetic makeup

– matatizo kwenye mfumo wa kinga mwili yaani autoimmune diseases,ambapo mfumo wa kinga mwili huanza kushambulia seli ndani ya mishipa ya damu, na moja ya vyanzo vya shida hii kutokea ni pamoja na;

  • maambukizi ya magonjwa kama vile homa ya ini-hepatitis B pamoja na hepatitis C
  • Saratani ya damu
  • magonjwa kwenye mfumo wa kinga mwili kama vile; rheumatoid arthritis, lupus pamoja na scleroderma

– Reactions kutokana na baadhi ya dawa n.k

Vitu ambavyo huongeza hatari ya mtu kupata Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu

– Umri, Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya Giant cell arteritis hutokea kabla ya miaka 50,

wakati Kawasaki disease hutokea zaidi kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5

– Family history, kuna na mgonjwa wa tatizo hili la kuvimba kwa mishipa ya damu ndani ya familia yako

– Matumizi ya cocaine pia huweza kuongeza hatari ya kupata Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu

– Uvutaji wa sigara au tumbaku(tobacco)

– matumizi ya baadhi ya dawa,

mfano wa dawa ni kama vile;

  • hydralazine,
  • allopurinol,
  • minocycline
  • pamoja na propylthiouracil.

– maambukizi ya magonjwa mbali mbali ikiwemo; Ugonjwa wa homa ya Ini(hepatitis B au C) pia huweza kuongeza hatari ya kupata Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu(vasculitis).

– Matatizo kwenye mfumo wa kinga mwilini(Immune disorders),

mfano magonjwa yanayohusisha mfumo wa kinga mwili kama vile;

  • lupus,
  • rheumatoid arthritis
  • Pamoja na scleroderma.

Matibabu ya Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu

matibabu ya Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu huhusisha zaidi kudhibiti hali ya kuvimba pamoja na dalili zinazojitokeza kwa mgonjwa baada ya kuvimba mishipa ya damu,

Zipo dawa mbali mbali ambazo huweza kutumika kwenye matibabu ya Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu, kama vile;

✓ Dawa jamii ya corticosteroid mfano; prednisone

✓ Dawa zingine ni pamoja na;

  •  methotrexate (Trexall),
  • azathioprine (Imuran, Azasan),
  • mycophenolate (CellCept),
  • cyclophosphamide,
  • tocilizumab (Actemra) au rituximab (Rituxan).

Hitimisho

Ni muhimu sana kufahamu dalili za Ugonjwa wa kuvimba kwa Mishipa ya damu, ili ukiona viashiria tu upate Msaada wa haraka zaidi,

Bila kuangalia aina moja moja,kwa Ujumla dalili za Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu ni pamoja na;

– mgonjwa Kupata homa

– Kupata maumivu ya kichwa

– Uzito wa mwili kupungua

– Kupata maumivu ya viungo,joints,misuli pamoja na mwili kwa ujumla

– Kama Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu umeathiri tumbo au utumbo, basi utapata maumivu baada ya kula chakula

– Kusababisha macho kuwa mekundu pamoja na kuwasha au kuhisi hali ya kuungua

– Baadhi ya aina za Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu(vasculitis) huweza kusababisha miguu kuchoma choma au kuwa dhaifu zaidi,

pia eneo la chini ya miguu pamoja na viganja vya mikono vinaweza kuvimba au kuwa vigumu zaidi.

– Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu unaweza kusababisha mtu kukosa pumzi au hata kukohoa damu kama umeathiri eneo la mapafu.

– Pia Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu unaweza kusababisha damu kuvuja chini ya ngozi kisha kupelekea madoa mekundu kuonekana kwenye ngozi(tazama mfano kwenye picha)

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.