Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Chanzo cha magonjwa ya figo pamoja na dalili zake

Chanzo cha magonjwa ya figo pamoja na dalili zake

Fahamu kuhusu Chanzo cha magonjwa ya figo pamoja na dalili zake kupitia kwenye makala hii.

Magonjwa ya Figo yamegawanyika kwenye makundi makubwa mawili(2),

  • Magonjwa ya muda mfupi(acute kidney diseases)
  • Pamoja na magonjwa ya kudumu (chronic kidney kideases)

Chanzo cha magonjwa ya figo

Zipo Sababu mbali mbali ambazo huweza kuwa Chanzo cha magonjwa ya figo, na Sababu hizo ni pamoja na;

– Kuwa na Ugonjwa wa kisukari(Type 1 au type 2 diabetes)

Ugonjwa wa kisukari huweza kuwa Chanzo cha magonjwa ya figo, kwani ugonjwa huu huweza kuongeza hatari zaidi ya mtu kuwa na matatizo ya figo

– Tatizo la shinikizo la juu la damu(High blood pressure)

Hii pia huweza kuwa Chanzo cha magonjwa ya figo

– Kuwa na tatizo la kuvimba kwa glomeruli yaani Glomerulonephritis

ambapo kazi yake kubwa ni kuchuja vitu mbali mbali kwenye figo

– Kuwa na tatizo la kuvimba kwa mirija kwenye figo yaani Interstitial nephritis

– Kuwa na magonjwa ya figo ya kurithi(inherited kidney diseases)

– Kuwa na tatizo kama vile Polycystic kidney disease

Vyote hivi huweza kuwa Chanzo cha magonjwa ya figo

– Kuwa na tatizo la kizuizi chochote cha muda mrefu kwenye njia ya mkojo,

Hii ni kutokana na matatizo kama vile;

  • Tatizo la kukua kwa tezi dume(enlarged prostate),
  • Kuwa na tatizo la mawe kwenye figo(kidney stones)
  • Au baadhi ya Saratani

Hali hii huweza kuwa Chanzo cha magonjwa ya figo

– Kuwa na tatizo la Vesicoureteral reflux, Tatizo ambalo hupelekea mkojo kurudi kwenye kibofu badala ya kutoka nje

– Kuwa na maambukizi ya vimelea vya magonjwa kwenye Figo ambayo hujirudia rudia mara kwa mara,

Hii pia ni miongoni mwa Chanzo cha magonjwa ya figo

Sababu ambazo huongeza hatari Zaidi ya kupata magonjwa ya figo

Hizi hapa ni baadhi ya sababu ambazo huongeza hatari zaidi ya mtu kupata magonjwa ya figo

1. Kuwa na Ugonjwa wa kisukari, Hii huweza kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya figo

2. Kuwa na tatizo la Presha ya kupanda, Hii pia huweza kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya figo

3. Kuwa na magonjwa mbali mbali ya moyo

4. Uvutaji wa Sigara

5. unywaji wa Pombe kupita kiasi

6. kuwa na tatizo la uzito mkubwa kupita kiasi(overweight/obesity)

Hii pia huweza kuongeza hatari ya wewe kupata magonjwa ya figo

7. Kuwa kwenye familia yenye historia ya kupata magonjwa ya figo

8. Kuwa na matatizo kwenye muundo au shape ya figo yaani Abnormal kidney structure

9. Kuwa na umri mkubwa zaidi

10. Matumizi ya dawa mara kwa mara,dawa ambazo huweza kuharibu figo

Vyote hivi hukuweka kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa ya figo

Dalili za magonjwa ya figo

magonjwa ya figo husababisha figo kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi, kulingana na jinsi figo zilivyoathirika,dalili mbali mbali huweza kujitokeza ikiwemo;

  • Kuhisi kichefuchefu pamoja kutapika
  • Kupoteza hamu ya kula
  • Mwili kuchoka kupita kiasi
  • Mwili kukosa nguvu na kuwa dhaifu sana
  • Kuwa na tatizo la kukosa usingizi
  • Kuwa na shida ya kukojoa zaidi au kutoa mkojo kidogo sana
  • Kuwa na shida ya misuli kukaza zaidi(Muscle cramps)
  • Kuwa na tatizo la Kuvimba MIGUU
  • ngozi kuwa kavu zaidi, kuwasha n.k

Hizo ndyo baadhi ya dalili za magonjwa ya figo

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.