Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Jinsi ya Kumkinga Mtoto tumboni na maambukizi ya Ugonjwa wa Kaswende

Ugonjwa wa kaswende kwa Mama Mjamzito huweza kupelekea maambukizi haya kupita hadi kwa mtoto na kisha kusababisha mtoto kuzaliwa na ugonjwa wa kaswende yaani kwa kitaalam hujulikana kama congenital syphilis

congenital syphilis ni Ugonjwa wa kaswende ambao hutokea baada ya mama mwenye Kaswende kupitisha maambukizi haya kwenda kwa mtoto wakati wa Ujauzito, hali ambayo hupelekea mtoto kuzaliwa na Ugonjwa wa kaswende.

Madhara ya Ugonjwa wa kaswende Kwa UJAUZITO

Ugonjwa wa kaswende kwa mama mjamzito huweza kusababisha;

  1. Mimba kutoka zenyewe(Miscarriage)
  2. Kuzaa mtoto ambaye tayari amefariki(Stillbirth)
  3.  Kuzaa mtoto kabla ya wakati au kuzaa mtoto njiti yaani Premature
  4. Kuzaa mtoto mwenye shida ya Uzito mdogo
  5. Kuzaa mtoto na kufa ndani ya muda mfupi baada ya kuzaliwa n.k

Madhara ya Ugonjwa wa kaswende Kwa Mtoto mwenyewe

Mtoto ambaye huzaliwa na Ugonjwa wa kaswende(Congenital syphilis) huweza kupata madhara mbali mbali ikiwemo;

– Mtoto kuwa na matatizo ya mifupa kama vile mifupa kuharibika au Deformed bones n.k,

– Mtoto kuwa na tatizo la upungufu mkubwa wa damu yaani Severe anemia

– Mtoto kuwa na tatizo la kuvimba Ini pamoja na bandama

– Mtoto kuwa na tatizo la Manjano(Jaundice)

– Mtoto kuwa na matatizo ya Ubongo pamoja na Nerva

– Mtoto kuwa na matatizo ya kutokuona au kutokusikia

– Mtoto kuwa na tatizo la Upele kwenye ngozi n.k

Jinsi ya Kumkinga Mtoto tumboni na maambukizi ya Ugonjwa wa Kaswende

Hizi hapa ni baadhi ya Njia za Jinsi ya Kumkinga Mtoto tumboni na maambukizi ya Ugonjwa wa Kaswende(congenital syphilis)

✓ Kwanza Fahamu kwamba Mtoto aliyetumboni hawezi kupata maambukizi ya ugonjwa wa kaswende kama mama mjamzito mwenyewe hana maambukizi haya,

Hivo jikinge kwanza wewe na maambukizi ya Ugonjwa wa kaswende pamoja na magonjwa mengine,ndipo na mtoto wako aliyetumboni atakuwa salama

✓ Hakikisha unafanya Vipimo vya Ugonjwa wa Kaswende Mara tu unapofika Hospital kwa ajili ya kuanza Kliniki kwenye hudhurio lako la kwanza(first visit)

✓ Hakikisha unajikinga na Ugonjwa wa Kaswende kabla ya Ujauzito na wakati wa ujauzito

✓ Hakikisha unajikinga na magonjwa mbali mbali yakiwemo magonjwa yote ya Zinaa

✓ Hakikisha unafanya Vipimo hata kabla ya kubeba mimba,kama unadalili za ugonjwa wa kaswende

✓ Baada ya kufanya Vipimo,endapo una ugonjwa wa kaswende hakikisha unapata tiba na kupona kabsa.

✓ Epuka tabia ya kuwa wapenzi wengi(Multiple sexual partners)

✓ Tumia kinga kama Condom wakati wa tendo la Ndoa n.k

Hizi ni baadhi ya Njia za Jinsi ya Kumkinga Mtoto tumboni na maambukizi ya Ugonjwa wa Kaswende

Kumbuka: Hata kama Ulipata Ugonjwa wa Kaswende kisha kupatiwa matibabu na kupona kabsa, Hii haimaanishi Ugonjwa huu wa Kaswende hauwezi kurudi tena, Hivo endelea kujilinda.

Hitimisho

Ugonjwa wa kaswende ni Ugonjwa ambao huweza kuleta madhara makubwa kwa Ujauzito pamoja na mtoto pia,

Madhara ya Ugonjwa wa kaswende kwa ujauzito ni pamoja na;

– Mimba kutoka zenyewe(Miscarriage)

– Kuzaa mtoto ambaye tayari amefariki(Stillbirth)

– Kuzaa mtoto kabla ya wakati au kuzaa mtoto njiti yaani Premature

– Kuzaa mtoto mwenye shida ya Uzito mdogo

– Kuzaa mtoto na kufa ndani ya muda mfupi baada ya kuzaliwa n.k

Madhara ya Ugonjwa wa kaswende Kwa Mtoto mwenyewe:

Mtoto ambaye huzaliwa na Ugonjwa wa kaswende(Congenital syphilis) huweza kupata madhara mbali mbali ikiwemo;

– Mtoto kuwa na matatizo ya mifupa kama vile mifupa kuharibika au Deformed bones n.k,

– Mtoto kuwa na tatizo la upungufu mkubwa wa damu yaani Severe anemia

– Mtoto kuwa na tatizo la kuvimba Ini pamoja na bandama

– Mtoto kuwa na tatizo la Manjano(Jaundice)

– Mtoto kuwa na matatizo ya Ubongo pamoja na Nerva

– Mtoto kuwa na matatizo ya kutokuona au kutokusikia

– Mtoto kuwa na tatizo la Upele kwenye ngozi n.k

Jinsi ya Kumkinga Mtoto tumboni na maambukizi ya Ugonjwa wa Kaswende

Hizi hapa ni baadhi ya Njia za Jinsi ya Kumkinga Mtoto tumboni na maambukizi ya Ugonjwa wa Kaswende(congenital syphilis)

✓ Kwanza Fahamu kwamba Mtoto aliyetumboni hawezi kupata maambukizi ya ugonjwa wa kaswende kama mama mjamzito mwenyewe hana maambukizi haya,

Hivo jikinge kwanza wewe na maambukizi ya Ugonjwa wa kaswende pamoja na magonjwa mengine,ndipo na mtoto wako aliyetumboni atakuwa salama

✓ Hakikisha unafanya Vipimo vya Ugonjwa wa Kaswende Mara tu unapofika Hospital kwa ajili ya kuanza Kliniki kwenye hudhurio lako la kwanza(first visit)

✓ Hakikisha unajikinga na Ugonjwa wa Kaswende kabla ya Ujauzito na wakati wa ujauzito

✓ Hakikisha unajikinga na magonjwa mbali mbali yakiwemo magonjwa yote ya Zinaa

✓ Hakikisha unafanya Vipimo hata kabla ya kubeba mimba,kama unadalili za ugonjwa wa kaswende

✓ Baada ya kufanya Vipimo,endapo una ugonjwa wa kaswende hakikisha unapata tiba na kupona kabsa.

✓ Epuka tabia ya kuwa wapenzi wengi(Multiple sexual partners)

✓ Tumia kinga kama Condom wakati wa tendo la Ndoa n.k

Hizi ni baadhi ya Njia za Jinsi ya Kumkinga Mtoto tumboni na maambukizi ya Ugonjwa wa Kaswende.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.