Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka,Soma hapa zaidi

jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka,Soma hapa zaidi

Fahamu kuhusu jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka ndani ya makala hii, hapa utapata tips mbali mbali za kukusaidia kama una tatizo hili.

Kumbuka, Mafuta mengi tumboni(Too much belly fat) huongeza hatari ya kupata magonjwa mbali mbali,

Moja ya njia muhimu za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka ni pamoja na;

  • kupunguza au kuacha kabsa matumizi ya Pombe,
  • Kufanya Mazoezi,
  • Pamoja na kula vyakula vya Protein zaidi.

jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka

Hizo hapa ni baadhi ya Tips za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka

1. Kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha nyuzi nyuzi zaidi(fiber)

Tafiti mbali mbali zinaonyesha kwamba,Nyuzi nyuzi au Fibers husaidia kupunguza Uzito hasa kwa kusababisha mtu kuhisi kushiba haraka na hivo kupunguza kiwango cha chakula anachokula,

Hivo moja ya njia za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka ni pamoja na kula vyakula vyenye fiber zaidi,

Hivi hapa ni vyanzo bora zaidi vya nyuzi nyuzi(Fibers);

  • Matunda mbali mbali kama vile maembe,machungwa n.k
  • Mboga za majani
  • Kunde
  • Shayiri n.k

2. Epuka ulaji wa vyakula vya mafuta mengi zaidi, Hii pia ni njia bora ya jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka

3. Dhibiti kabsa matumizi ya Pombe,

Pombe ni moja ya vitu ambavyo vinavyochangia kwa kiasi kikubwa tumbo kuwa kubwa(belly fat),

mbali na hivo,Pombe husababisha kwa kiasi kikubwa tatizo la Uzito mkubwa(overweight).

Hivo basi,kupunguza matumizi ya Pombe ni mojawapo ya njia za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka.

4. Kula vyakula vya proteins zaidi,

Proteins ni kirutubisho muhimu kwa ajili ya kusaidia kupunguza Uzito na tumbo kwa ujumla,

Hii ni kwa Sababu, Proteins huongeza uzalishwaji wa kichocheo kinachojulikana kama “fullness hormone peptide YY”,

ambacho husaidia kupunguza hamu ya chakula, na kusababisha mtu kushiba kwa haraka zaidi.

Hivo basi, Ulaji wa vyakula vya Proteins zaidi ni mojawapo ya njia za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka

Hivi ni baadhi ya vyanzo mbali mbali vya Proteins;

  • Nyama
  • Samaki
  • mayai
  • Maziwa
  • Maharage n.k

5. Hakikisha unadhibiti Tatizo la Msongo wa mawazo,

Watu wengi hawajui kwamba Stress huweza kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha mafuta tumboni yaani belly fat ,

Hii ni kutokana na Kusababisha tezi la adrenal glands kuzalisha hormones ambazo hujulikana kama cortisol au stress hormone.

Tafiti zinaonyesha,Kiwango kikubwa cha cortisol huongeza hamu ya kula zaidi, na kuongeza mafuta zaidi tumboni.

6. Epuka kula vyakula vya Sukari zaidi,

Tumia Sukari kwa kiasi,

7. Fanya Mazoezi mbali mbali ya mwili,

Kama tunavyofahamu moja ya njia bora zaidi ya kupunguza Uzito ni pamoja na kufanya mazoezi,

Hivo basi, unaweza kupunguza mafuta ya tumboni kwa njia ya kufanya mazoezi-aerobic exercise (cardio),

Mazoezi ni mojawapo ya njia bora zaidi za kupunguza tumbo kwa haraka.

8. Pata muda wa kutosha wa kulala

Baadhi ya tafiti zinaonyesha,uhusiano wa mtu kutokulala au kutokupata usingizi wa kutosha na tatizo la Unene/ obesity pamoja na kuongeza kiwango cha mafuta tumboni Yaani belly fat,

Hivo basi, kupata muda wa kutosha wa kulala vizuri ni mojawapo ya njia za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka.

9. Tumi Samaki wenye mafuta

Moja ya njia za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka ni pamoja na ulaji wa samaki wa mafuta kila wiki,
Samaki wana kiwango kikubwa cha protein bora zaidi pamoja na omega-3 fats,

Tafiti zinaonyesha omega-3 fats huweza kusaidia kupunguza mafuta ambayo kwa kitaalam tunaita visceral fat.

10. Dhibiti kiwango cha matumizi ya Juice za matunda yaani fruit juice,

Ingawa Juice za matunda ni bora zaidi na zina vitamins pamoja na madini ya kutosha, bado huweza kuwa kwenye kundi la Vitu vyenye kiwango kikubwa cha Sukari kama vile Soda pamoja na vinywaji vingine.

Baadhi ya tafiti zinaonyesha matumizi makubwa ya juice za matunda huweza kusababisha mtu kuongezeka uzito wa mwili, hii ni kwa sababu ya kiwango kikubwa cha Calories kutoka kwa Juice hizi.

Hivo basi,Moja ya njia za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka ni pamoja na kupunguza matumizi ya Juice za matunda.

11. funga kwa vipindi au tunaita intermittent fasting

Kufunga ni mojawapo ya njia maarufu ambayo watu wengi hutumia ili kupunguza uzito,

Ingawa unatakiwa kuwa makini na Njia hii ili usije kusababisha matatizo mengine ya kiafya kama vile vidonda vya tumbo n.k

Kwa upande wa Intermittent fasting,Mtu hushauriwa kufunga au kuacha kula kwa baadhi ya milo na kisha kula kwa baadhi ya milo mingine.

Wengi hutumia kanuni hii ya jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka kwa Njia ya Kufunga;

  • Njia moja maarufu inahusisha kufunga kwa saa 24 mara moja au mbili kwa juma(wiki).
  • Na Nyingine ni kufunga kila siku kwa masaa 16 na kula chakula chako chote ndani ya kipindi cha masaa 8.

12. Kunywa chai ya kijani au green tea

Green tea ni kinywaji ambacho kina faida nyingi sana kiafya,ikiwemo hii ya kusaidia watu wenye matatizo ya Uzito mkubwa,tumbo kubwa n.k

Ingawa huwezi kutumia green tea peke yake ukapungua uzito,lazima utumie pamoja na njia nyingine za kupunguza uzito kama vile kufanya mazoezi n.k

Hitimisho

Kuna Njia mbali mbali za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka, njia hizo ni pamoja na kufanya Mazoezi mbali mbali,kuepuka vyakula vya mafuta mengi badala yake kula vyakula vya Proteins pamoja na nyuzi nyuzi zaidi,

Dhibiti matumizi ya Pombe, Sukari nyingi, pata muda wa kutosha wa kulala,punguza msongo wa mawazo n.k

Hizo ni baadhi ya Njia za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.