Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Magonjwa yatokanayo na lishe duni,Soma hapa kufahamu

Magonjwa yatokanayo na lishe duni,Soma hapa kufahamu

Katika Makala hii tumechambua Magonjwa yatokanayo na lishe duni,Soma hapa kufahamu.

Magonjwa yatokanayo na lishe duni

Hapa tunazungumzia magonjwa yote yanayotokana na mtu kutopata Lishe bora(unhealth diet),

Lishe duni, hatumaanishi upungufu wa chakula pekee, bali tunamaanisha pia kukosa mlo wenye Virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kwa kiwango sahihi.

Magonjwa yatokanayo na lishe duni ni mengi, Ikiwemo magonjwa kama vile;

  • Tatizo la Utapiamlo
  • Tatizo la unene na Uzito kupita kiasi(Overweight&obesity)
  • Magonjwa ya Moyo
  • Kiharusi(Stroke)
  • Kisukari aina ya pili(type 2 diabetes)
  • Saratani mbali mbali n.k

Lishe isiyofaa au Lishe duni ni sababu mojawapo ya mtu kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa mengi sugu,

Kupata lishe ya kutosha ni sehemu muhimu ya kuishi maisha yenye afya, Lishe duni inaweza kutokana na kushindwa kula chakula cha kutosha au kushindwa kuchagua aina sahihi za vyakula.

Magonjwa yatokanayo na lishe duni

Magonjwa yatokanayo na lishe duni ni pamoja na;

1. Kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya Moyo

2. Tatizo la kiharusi au Stroke

3. Kupata Ugonjwa wa Kisukari

4. Kupata matatizo kama vile arthritis

5. Kuwa kwenye hatari ya kupata Ugonjwa wa UTAPIAMLO, Tatizo hili ni miongoni mwa Magonjwa yatokanayo na lishe duni.

6. Kuwa kwenye hatari ya kupata Saratani za aina mbali mbali

7. Kupata tatizo la Presha, kiwango kikubwa cha lehemu au cholestrol mwilini n.k

8. Ugonjwa wa Anemia, pia upungufu wa damu au anemia huweza kuwa miongoni mwa Magonjwa yatokanayo na lishe duni,

Anemia ina sababu mbalimbali, na baadhi ya sababu hizo ni kuhusiana na upungufu wa baadhi ya virutubisho mwilini kama vile;

  • Madini ya Chuma(Iron).
  • Upungufu wa vitamin B12, n.k

9. Kupata Ugonjwa wa Matege pamoja na mifupa kwa ujumla( Rickets)

Tatizo la matege ni miongoni mwa Magonjwa yatokanayo na lishe duni, Matege hutokana na upungufu mkubwa wa Virutubisho muhimu mwilini ikiwemo;

  • vitamin D,
  • calcium
  • Au phosphate.

10. Ugonjwa wa Sukari aina ya pili(Type 2 diabetes) huweza kuwa miongoni mwa Magonjwa yatokanayo na lishe duni,

Ikiwa mlo wako hauna virutubisho– kama vile protini, wanga, mafuta, vitamini na madini — unaweza kuwa na utapiamlo. Utapiamlo hutokea katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea.

11. Ugonjwa wa Kwashiorkor
Kwashiorkor ni miongoni mwa Magonjwa yatokanayo na lishe duni,

ni ugonjwa unaosababishwa na utapiamlo au kutokula lishe bora. Ugonjwa huu mara nyingi hutokea katika maeneo ambayo yamekumbwa na ukame au njaa, na hutokea wakati hakuna protini ya kutosha katika mlo wa mtu.

12. Tatizo la Osteomalacia
Osteomalacia ni miongoni mwa Magonjwa yatokanayo na lishe duni,

ni hali inayohusiana na mifupa ambayo inahusishwa na lishe isiyofaa. Osteomalacia kwa kawaida hutokana na upungufu wa vitamini D;

“Lishe duni inaweza kuchangia msongo wa mawazo, uchovu na uwezo wetu wa kufanya kazi kupungua, na baada ya muda, inaweza kuchangia hatari ya kupata magonjwa na matatizo mengine ya afya kama vile:

✓ kuwa na tatizo la Uzito mkubwa au mnene kupita kiasi

✓ kuoza kwa meno

✓ kupata shinikizo la damu

✓ Kiwango cha cholesterol kuwa juu

✓ Ugonjwa wa moyo na kiharusi

✓ kisukari aina ya 2

✓ Kupata tatizo la osteoporosis

✓ Kupata baadhi ya saratani

✓ Kuwa na shida ya huzuni

✓ kupata matatizo ya kula,(eating disorders).”

Hitimisho

Hayo ndyo baadhi ya Magonjwa yatokanayo na lishe duni.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.