Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Vidokezo vya Kukusaidia kama Unasumbuliwa na UTI za mara kwa mara

Vidokezo vya Kukusaidia kama Unasumbuliwa na UTI za mara kwa mara

Je Uasumbuliwa na UTI za mara kwa mara? Fahamu baadhi ya Vidokezo vya Kukusaidia kama Unasumbuliwa na UTI za mara kwa mara,

soma Zaidi hapa..!!!

Unaweza kuwa na maambukizi kwenye njia ya mkojo ambayo hujirudia mara kwa mara pasipo kujua nini kinasababisha hasa,

Tatizo la UTI huhusisha mashambulizi ya bacteria kwenye mfumo mzima wa mkojo ikiwemo;

  • Kibofu cha mkojo
  • Figo
  • Njia ya Mkojo n.k

Vidokezo vya Kukusaidia kama Unasumbuliwa na UTI za mara kwa mara

Hivi hapa ni baadhi ya Vidokezo vya Kukusaidia kama Unasumbuliwa na UTI za mara kwa mara;

1. Hakikisha Usafi wa Choo unachotumia

Hapa nazungumzia mazingira ya chooni kwa ujumla,

ikiwemo;

  • Usafi wa maji unayotumia
  • Usafi wa vyombo
  • Pamoja na Choo kwa Ujumla

2. Hakikisha unakunywa maji ya kutosha, Hii ni mojawapo ya Vidokezo vya Kukusaidia kama Unasumbuliwa na UTI za mara kwa mara,

Kunywa maji kuanzia lita 2.5 na kuendelea kwa siku huweza kupunguza maambukizi ya UTI kwa zaidi ya asilimia 50%,

kumbuka; ukinywa maji mengi itasababisha ukojoe mara kwa mara, na hii itasaidia kuflash bacteria kutoka kwenye njia ya mkojo kabla ya maambukizi kuanza.

3. Pendelea kutumia juice mbali mbali za matunda ikiwemo Juice ya cranberry juice.

4. Jisafishe kutoka mbele kwenda Nyuma(Wipe from front to back).

Hii ni mojawapo ya Vidokezo vya Kukusaidia kama Unasumbuliwa na UTI za mara kwa mara,

Baadhi ya watu hasa wanawake,kutokana na maambilie yao yalivyo hupata UTI wakati wa kujisafisha baada ya kujisaidia haja kubwa,

Unapojisafisha kutoka nyuma kwenda mbele,unaweza kuhamisha bacteria kutoka sehemu ya haja kubwa kisha kupeleka sehemu ya haja ndogo,

Hivo basi kujisafisha kutoka mbele kwenda nyuma itasaidia kuzuia kusambaza bacteria kutoka kwenye sehemu ya haja kubwa kwenda ukeni pamoja na kwenye njia ya mkojo kwa ujumla.

5. Kojoa mara tu baada ya kufanya tendo la ndoa,

Unashauriwa kukojoa mara tu baada ya tendo la ndoa,Pia Kunywa maji mengi ili kusaidia kuflash bacteria.

6. Epuka matumizi ya vitu vyenye kemikali Zaidi sehemu za Siri,

Hapa nazungumzia vitu kama vile;

  • Baadhi ya Sabuni za Kuogea
  • deodorant sprays,
  • douches
  • powders
  • Mafuta n.k.

7. Badili baadhi ya njia za kuzuia mimba,

Hapa nazungumzia vitu kama vile Diaphragms, condom ambazo hazijatengenezwa na vilainishi(unlubricated condoms) au matumizi ya condoms ambazo zina spermicide ndani yake, Hii inaweza kupelekea bacteria kukua zaidi.

Hivo ni baadhi ya Vidokezo vya Kukusaidia kama Unasumbuliwa na UTI za mara kwa mara.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.