Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Watoto wa kiume waliozaliwa na akina mama walio na COVID-19 kupata matatizo ya ubongo

Watoto wa kiume waliozaliwa na akina mama walio na COVID-19 kupata matatizo ya ubongo

Watoto wa kiume waliozaliwa na akina mama walio na COVID-19 wanaweza kukabili matatizo ya ukuaji wa ubongo kwa kiwango cha mara mbili zaidi ya wengine, utafiti mpya uligundua.

Utafiti huo ulihusisha zaidi ya watoto 18,000 waliozaliwa katika hospitali nane huko Massachusetts. Takriban 900 kati yao walizaliwa na wanawake ambao walikuwa na COVID-19 wakiwa wajawazito.

Watoto wa kiume walikabiliwa zaidi na matatizo mbalimbali ya ukuaji katika miezi 18 ya kwanza ya maisha, unasema utafiti huo, ambao ulichapishwa katika jarida la “JAMA Network Open”,ambalo Lilichambua rekodi za afya za kielektroniki.

Masuala hayo yalijumuisha ucheleweshaji wa kuongea/lugha kwa watoto, maendeleo ya kisaikolojia, utendaji pamoja na uwezo wa kiakili,

Au tunasema;

  • delays in speech and language,
  • psychological development,
  • motor function
  • and intellectual abilities.

Matatizo hayo yanaweza kuhusishwa na tatizo la Usonji(autism) miongoni mwa watoto wakubwa, lakini “ni mapema sana kusema tatizo ni Usonji” kwa watoto waliofanyiwa utafiti, Roy Perlis, MD, aliiambia NPR.

Perlis ni mwandishi mwenza wa ripoti hiyo na daktari wa magonjwa ya akili katika Hospitali Kuu ya Massachusetts.

“Tunachoweza kugundua katika hatua hii ni matatizo zaidi kama vile ucheleweshaji wa lugha na kuongea, pamoja na ucheleweshaji wa hatua muhimu za kiutendaji yaani motor milestones,” alisema.

“Watoto wengi waliozaliwa na akina mama ambao wana COVID wakati wa ujauzito hawatakuwa na athari za ukuaji yaani neurodevelopmental hata kama kuna ongezeko fulani la hatari.”

#Tafiti

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.