Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kwanini hakuna Vidonge vya majira kwa wanaume?

Kwanini hakuna Vidonge vya majira kwa wanaume?

Ni kwa muda sasa watu wamekuwa wakitumia au kusikia kuhusu vidonge vya majira au vya uzazi wa mpango kwa wanawake,

Je ni kwanini hakuna Vidonge vya Uzazi wa mpango kwa Wanaume?

Utafiti unaonyesha kuwa wanaume wengi wangefurahia uchaguzi wa vidonge vya kudhibiti uzazi kuliko njia nyingine kama vile kufunga kabsa uzazi, Kulingana na unayemuuliza, hadi asilimia 83% ya wanaume wanasema wataitumia.

Lakini kupata vidonge vya kupanga uzazi kwa wanaume ambavyo ni salama, vya kuaminika na vyenye ufanisi wa kudhibiti Ujauzito bado ni changamoto kubwa,

Sayansi ya Kudhibiti mwanaume kutungisha mimba kwa njia ya vidonge bado ni ngumu, Ili kidonge kiwe na ufanisi, watafiti hutafuta kufanya angalau moja ya mambo machache:

  1. Lazima kiwe na uwezo wa kupunguza au kuzuia utengenezaji wa mbegu za kiume
  2. Au Lazima kiwe na uwezo wa kuzuia mbegu za kiume kutoka kwa Mwanaume
  3. Au kiwe na uwezo wa kupunguza kasi ya Mbegu za kiume, Kupunguza kasi ya manii ili kuzuia kufika kwenye yai,kisha kuzuia kurutubisha yai.

Kufikia sasa, majaribio mengi katika hili yamekuwa ya sindano, sio vidonge. Hiyo sio bora.

Vidonge vingine vinavyotengenezwa vinaweza kuleta matatizo kwenye ini lako, Na madhara mengine — mambo kama chunusi, kuongezeka uzito, mabadiliko katika hamu ya tendo la ndoa, na mabadiliko ya hisia — yanaweza kutokea, pia.

Mpaka Sasa bado tafiti zinaendelea kuhusu Vidonge vya majira au Vidonge vya Uzazi kwa wanaume.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.