Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora

Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora

Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora,Soma hapa kufahamu

Katika Makala hii tumechambua Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora,Soma hapa kufahamu.

Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora

Hapa tunazungumzia Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora

Ukosefu wa Lishe bora, hatumaanishi upungufu wa chakula pekee, bali tunamaanisha pia kukosa mlo wenye Virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kwa kiwango sahihi.

Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora ni mengi, Ikiwemo magonjwa kama vile;

  • Tatizo la Utapiamlo
  • Tatizo la unene na Uzito kupita kiasi(Overweight&obesity)
  • Magonjwa ya Moyo
  • Kiharusi(Stroke)
  • Kisukari aina ya pili(type 2 diabetes)
  • Saratani mbali mbali n.k

Lishe isiyofaa au Lishe duni ni sababu mojawapo ya mtu kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa mengi sugu,

Kupata lishe bora na ya kutosha ni sehemu muhimu ya kuishi maisha yenye afya, Ukosefu wa Lishe bora huweza kutokana na mtu kushindwa kuchagua aina sahihi za vyakula.

Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora

Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora ni pamoja na;

1. Kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya Moyo

2. Tatizo la kiharusi au Stroke

3. Kupata Ugonjwa wa Kisukari

4. Kupata matatizo kama vile arthritis

5. Kuwa kwenye hatari ya kupata Ugonjwa wa UTAPIAMLO, Tatizo hili ni miongoni mwa Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora.

6. Kuwa kwenye hatari ya kupata Saratani za aina mbali mbali

7. Kupata tatizo la Presha, kiwango kikubwa cha lehemu au cholestrol mwilini n.k

8. Ugonjwa wa Anemia, pia upungufu wa damu au anemia huweza kuwa miongoni mwa Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora

Anemia ina sababu mbalimbali, na baadhi ya sababu hizo ni kuhusiana na upungufu wa baadhi ya virutubisho mwilini kama vile;

  • Madini ya Chuma(Iron).
  • Upungufu wa vitamin B12, n.k

9. Kupata Ugonjwa wa Matege pamoja na mifupa kwa ujumla( Rickets)

Tatizo la matege ni Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora,Matege hutokana na upungufu mkubwa wa Virutubisho muhimu mwilini ikiwemo;

  • vitamin D,
  • calcium
  • Au phosphate.

10. Ugonjwa wa Sukari aina ya pili(Type 2 diabetes) huweza kuwa miongoni mwa Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora

Ikiwa mlo wako hauna virutubisho– kama vile protini, wanga, mafuta, vitamini na madini — unaweza kuwa na utapiamlo. Utapiamlo hutokea katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea.

11. Ugonjwa wa Kwashiorkor
Kwashiorkor ni miongoni mwa Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora

ni ugonjwa unaosababishwa na utapiamlo au kutokula lishe bora. Ugonjwa huu mara nyingi hutokea katika maeneo ambayo yamekumbwa na ukame au njaa, na hutokea wakati hakuna protini ya kutosha katika mlo wa mtu.

12. Tatizo la Osteomalacia
Osteomalacia ni miongoni mwa Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora

ni hali inayohusiana na mifupa ambayo inahusishwa na lishe isiyofaa. Osteomalacia kwa kawaida hutokana na upungufu wa vitamini D;

“Ukosefu wa Lishe bora unaweza kuchangia msongo wa mawazo, uchovu na uwezo wetu wa kufanya kazi kupungua, na baada ya muda, inaweza kuchangia hatari ya kupata magonjwa na matatizo mengine ya afya kama vile:

✓ kuwa na tatizo la Uzito mkubwa au mnene kupita kiasi

✓ kuoza kwa meno

✓ kupata shinikizo la damu

✓ Kiwango cha cholesterol kuwa juu

✓ Ugonjwa wa moyo na kiharusi

✓ kisukari aina ya 2

✓ Kupata tatizo la osteoporosis

✓ Kupata baadhi ya saratani

✓ Kuwa na shida ya huzuni

✓ kupata matatizo ya kula,(eating disorders).”

Hitimisho

Hayo ndyo baadhi ya Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora,

Kumbuka lishe bora ni dawa na kinga dhidi ya magonjwa mbali mbali.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.