Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Nimesikitishwa Sana na taarifa ya kifo cha Dkt. Isack Sima-Mhe. Ummy Mwalimu

Nimesikitishwa Sana na taarifa ya kifo cha Dkt. Isack Sima-Mhe. Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Dkt. Isack Sima aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyangoto, kilichopo Wilaya ya Tarime Vijijini, Mkoa wa Mara ambaye inadaiwa ameuawa tarehe 03 May, 2023 kwa kukatwakatwa na mapanga na Watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake akitokea kazini.

Waziri Ummy amelaani vikali kitendo hicho cha mauaji ya Mwanataaluma ya Udaktari ambacho hakikubaliki katika Jamii ambapo ametoa pole nyingi kwa Ndugu, Jamaa, Marafiki, Watumishi wote wa Sekta ya Afya Tarime, na Wanataaluma Nchini kwa ujumla na Watu wote walioguswa kutokana na mauaji haya.

Ummy amenukuliwa akisema “Tunaamini Vyombo vya Dola vitafanikisha kupatikana kwa Wahusika waliofanya kitendo hiki”

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.