Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Fahamu zaidi Kuhusu Virusi hivi vya Norovirus, dalili na jinsi ya kujikinga navyo

Fahamu zaidi Kuhusu Virusi hivi vya Norovirus, dalili na jinsi ya kujikinga navyo

Norovirus ni virusi vinavyoambukiza sana na vinavyosababisha mtu kutapika na kuharisha,

Mtu yeyote anaweza kuambukizwa virusi hivi vya norovirus.

Virusi vya Norovirus kwa jina lingine hujulikana kama “stomach flu” au “stomach bug”.

Hata hivyo, ugonjwa unaotokana na virusi vya norovirus hauhusiani na mafua, ambayo husababishwa na virusi vya mafua. 

Fahamu Zaidi kuhusu dalili za norovirus, jinsi virusi hivi huenea, na jinsi ya kuzuia norovirus.

Dalili za maambukizi ya Norovirus

Dalili za maambukizi ya Norovirus ni pamoja na;

1. Mtu kuharisha

2. Mtu kutapika

3. Mtu kuhisi kichefuchefu kila mara

4. Mtu kupata maumivu ya tumbo n.k

Jinsi ya kujikinga na maambukizi ya norovirus

Jilinde mwenyewe na wengine kutoka kwa norovirus kwa kufanya haya;

✓ Nawa mikono mara kwa mara

✓ Osha vizuri matunda kabla ya kula

✓ Osha vizuri mboga za majani kabla ya kuanza kupika

✓ Hakikisha unapika samaki vizuri

✓ Kaa nyumbani wakati unaumwa

✓ kaa nyumbani angalau kwa siku mbili baada ya dalili kuacha kujitokeza

✓ Epuka kuandalia wengine chakula kama tayari unaumwa.

#norovirus

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.