Idadi ya wazee imeongezeka kutoka 2,507,568 mwaka 2012 hadi kufikia 5,008,339 mwaka 2022
Idadi ya wazee imeongezeka kutoka 2,507,568 mwaka 2012 hadi kufikia 5,008,339 mwaka 2022
“Maadhimisho ya Kupinga ukatili Dhidi ya Wazee hufanyika tarehe 15 Juni, Kila mwaka. Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Wazee Wanastahili Heshima na Usikivu Wetu”.
Maadhimisho haya yatafanyika katika ngazi ya Mikoa kote nchini- Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa @maendeleoyajamii
Waziri Dkt. Gwajima amebainisha kuwa
kutokana na kuboreshwa kwa huduma mbalimbali za kijamii nchini idadi ya wazee imeongezeka kutoka 2,507,568 mwaka 2012 hadi kufikia 5,008,339 mwaka 2022 ambayo ni sawa na asilimia 8.1 ya Watanzania 61,741,120.
“Serikali imeendelea kuadhimisha Siku ya kupinga Ukatili Dhidi ya Wazee kila mwaka ambapo katika kulinda haki ya wazee kuishi, pia imeendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji kwa Wazee”- Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa @maendeleoyajami