Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

jinsi ya kupima BMI, soma hapa kufahamu

jinsi ya kupima BMI, soma hapa kufahamu

BMI Ni kifupi cha “Body Mass Index” ambapo huhusisha mahesabu rahisi ya Kutumia Uzito(weight) wa Mtu pamoja na Urefu wa mtu(height),

ili kujua Uzito halisi wa Mtu upo kwenye kiwango gani, na kwa kutumia BMI ndipo tunapoweza kutoa Majibu kwamba;

  • Mtu huyu ana Uzito mkubwa kupita kiasi(overweight),
  • Mtu huyu ana uzito wa kawaida(Normal weight),
  • Mtu huyu ana uzito mdogo sana(underweight) n.k.

Formula ya BMI = kg/m2 ambapo “kg” ni kipimo cha uzito wa mtu kwenye kilograms na “m2” ni kipimo cha urefu wa mtu kwenye metres squared,

Hivo basi,ili kupata majibu ya BMI unachukua Uzito wa Mtu kwenye (Kg) kugawanya Urefu wa Mtu kwenye(m2).

Mfano; Mtu mzima mwenye Uzito wa kilogram(kg) 70 ambaye urefu wake ni Metres(m) 1.75 atakuwa na BMI ya 22.9.

70 (kg)/1.752 (m2) = 22.9 BMI.

Majibu ya BMI yakiwa 25.0 au Zaidi basi una uzito mkubwa au overweight, wakati Majibu ya BMI yakiwa 18.5 mpaka 24.9 basi una uzito wa kawaida ambao unatakiwa kiafya(healthy weight/normal weight).

BMI hutumika Zaidi kwa watu wenye umri wa Miaka 18-65.

Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO)

“kwa Mtu Mzima mwenye Miaka zaidi ya 20, BMI yake itakuwa kama ifuatavyo;”

Kwa watu wazima zaidi ya umri wa miaka 20, BMI iko katika mojawapo ya makundi yafuatayo.

Table 1. Nutritional status

BMI Nutritional status
Below 18.5 Underweight
18.5–24.9 Normal weight
25.0–29.9 Pre-obesity
30.0–34.9 Obesity class I
35.0–39.9 Obesity class II
Above 40 Obesity class III

Summary;

(1) Majibu ya BMI yakiwa 25.0 au Zaidi basi una uzito mkubwa au overweight,

(2) wakati Majibu ya BMI yakiwa 18.5 mpaka 24.9 basi una uzito wa kawaida ambao unatakiwa kiafya(healthy weight/normal weight),

(3) Lakini Majibu ya BMI yakiwa chini ya 18.5 basi una Uzito mdogo(Underweight)

Je,ni Watu gani hawaruhusiwi kutumia BMI calculator?

Kundi hili la Watu linashauriwa kutokutumia BMI kwani majibu yanaweza yasiwe Sahihi kwao;

– BMI isitumike kwa wajenga misuli(muscle builders),

– wanariadha wa masafa mareful(Long distance athletes),

– Wakina mama wajawazito(pregnant women),

– Wazee au watoto wadogo(the elderly or young children).

  • Hii ni kwa sababu BMI haizingatii ikiwa uzito unabebwa kama misuli au mafuta, bali namba tu.
  • Wale walio na misuli mikubwa(higher muscle mass), kama vile wanariadha, wanaweza kuwa na BMI ya juu lakini wasiwe katika hatari kubwa ya kiafya.
  • Wale walio na misuli midogo(lower muscle mass), kama vile watoto ambao bado wapo kwenye hatua za ukuaji au wazee ambao wanaweza kupoteza misuli fulani wanaweza kuwa na BMI ya chini.
  • Wakati wa ujauzito na Unyonyeshaji, muundo wa mwili wa mwanamke hubadilika, hivyo kutumia BMI sio sahihi.

Hitimisho

BMI Ni kifupi cha “Body Mass Index” ambapo huhusisha mahesabu rahisi ya Kutumia Uzito(weight) wa Mtu pamoja na Urefu wa mtu(height),ili kujua Uzito halisi wa Mtu upo kwenye kiwango gani.

Mfano;

(1) Majibu ya BMI yakiwa 25.0 au Zaidi basi una uzito mkubwa au overweight,

(2) wakati Majibu ya BMI yakiwa 18.5 mpaka 24.9 basi una uzito wa kawaida ambao unatakiwa kiafya(healthy weight/normal weight),

(3) Lakini Majibu ya BMI yakiwa chini ya 18.5 basi una Uzito mdogo(Underweight)

Lakini Pia,Kundi hili la Watu linashauriwa kutokutumia BMI kwani majibu yanaweza yasiwe Sahihi kwao;

– BMI isitumike kwa wajenga misuli(muscle builders),

– wanariadha wa masafa mareful(Long distance athletes),

– Wakina mama wajawazito(pregnant women),

– Wazee au watoto wadogo(the elderly or young children).

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.