Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kangaroo mother care (KMC), kupunguza Vifo vya watoto waliozaliwa na Uzito mdogo

Kangaroo mother care (KMC), kupunguza Vifo vya watoto waliozaliwa na Uzito mdogo

Kangaroo mother care (KMC), huhusisha mgusano wa karibu wa ngozi kwa ngozi kati ya akina mama na watoto wao wachanga waliozaliwa na uzito mdogo,

(Tazama mfano kwenye picha hii)

Kangaroo mother care (KMC),inaonekana kupunguza hatari ya vifo vya watoto waliozaliwa na uzito mdogo kwa karibu theluthi moja ukilinganisha na utunzaji wa kawaida kwa Watoto hawa, Hii ni kulingana na utafiti mpya uliochapishwa kwenye jarida la “BMJ Global Health”.

Kuanzisha mawasiliano ya karibu(close skin-to-skin contact) ambayo yanahusisha akina mama kubeba mtoto mchanga katika kombeo, ndani ya saa 24 baada ya kuzaliwa na kuendelea kwa angalau saa 8 kwa siku zote mbili zinaonekana kuongeza matokeo chanya katika kupunguza vifo na maambukizi kwa Watoto waliozaliwa na Uzito mdogo.

Utafiti ulihusisha majaribio 31 ambayo yalijumuisha watoto 15,559 waliozaliwa na Uzito mdogo pamoja na watoto waliozaliwa kabla ya wakati kwa pamoja,

Kati ya majaribio 31, tafiti 27 zililinganisha Kangaroo Mother Care(KMC )na utunzaji wa kawaida kwa watoto hawa,

Wakati nne zilizobaki zikilinganisha kati ya kuanza mapema na kuchelewa kuanza kwa kangaroo mother care(KMC).

Kupunguza hatari ya vifo

Uchambuzi ulionyesha kuwa, ikilinganishwa na utunzaji wa kawaida, Kangaroo Mother Care(KMC) ilionekana kupunguza hatari ya vifo kwa asilimia 32% wakati wa kulazwa hospitalini au kwa siku 28 baada ya watoto hawa kuzaliwa,

Pia ilionekana kupunguza hatari ya maambukizi makali, kama vile sepsis, kwa asilimia15%.

kupungua kwa hatari ya vifo kwa Watoto hawa wenye uzito mdogo na kuzaliwa kabla ya wakati(premature) kulionekana bila kujali umri wa ujauzito au uzito wa mtoto wakati wa kuandikishwa, wakati wa kuanza kangaroo mother care(KMC), wala ikiwa Kangaroo mother care(KMC) ilianzishwa hospitalini au nyumbani.

Tafiti zilizolinganishwa ikiwa KMC iliyochelewa kuanzishwa zilionyesha kupungua kwa vifo vya watoto wachanga kwa asilimia 33%.

Nchi zenye kipato cha chini na cha kati zina viwango vya juu zaidi vya Watoto kuzaliwa kabla ya wakati (umri wa ujauzito ukiwa chini ya wiki 37) na Watoto kuzaliwa na uzito mdogo (chini ya gramu 2,500),

Watoto Kuzaliwa kabla ya wakati(premature) na kuzaliwa wakiwa na uzito mdogo(low-birth weight) vyote hivi ni sababu kuu za kifo na ulemavu kwa Watoto.

Shirika la Afya Duniani(WHO) linapendekeza Kangaroo Mother Care(KMC) kama standard of care kwa watoto wachanga waliozaliwa na uzito mdogo.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.