Kenya imeweka historia kwa kuandaa Mazungumzo ya Kitaifa yanayohusu Ufadhili wa Afya(National Health Financing Dialogue)
Kenya imeweka historia kwa kuandaa Mazungumzo ya Kitaifa yanayohusu Ufadhili wa Afya(National Health Financing Dialogue)
Kenya imeweka historia kwa kuandaa Mazungumzo ya Kitaifa ya Ufadhili wa Afya “National Health Financing Dialogue”,
na kuwa nchi ya kwanza ya Afrika Mashariki na ya tatu barani Afrika kuandaa hafla hii muhimu.
Mazungumzo hayo yalilenga kushughulikia masuala muhimu ya ufadhili endelevu katika sekta ya afya na kubuni mikakati madhubuti ya utekelezaji.
Wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa kitaifa wa ngazi ya juu kuhusu Huduma ya Afya kwa Wote (UHC), ulioongozwa na Waziri Mkuu Musalia Mudavadi kwa niaba ya Rais William Ruto, Waziri wa Baraza la Mawaziri Nakhumicha S. Wafula alisisitiza dhamira ya serikali ya kuweka mfumo wa huduma ya afya nchini Kenya katika hali endelevu.
Aliangazia ongezeko kubwa la mgao wa bajeti kwa afya katika miaka ya hivi karibuni, akionyesha ari kubwa ya serikali katika kuweka kipaumbele katika huduma za afya.
Waliohudhuria walikuwa viongozi, wakiwemo maafisa kutoka Wizara ya Afya, Makatibu Wakuu @KimtaiHarry na @muthonikenya, pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Magavana (COG), @AnneWaiguru, miongoni mwa wengine.
Kenya made history today by hosting the National Health Financing Dialogue, becoming the first East African country and the third in Africa to organize this crucial event. The dialogue aimed to address pressing issues of sustainable financing in the healthcare sector and devise… pic.twitter.com/mGx4abq6wL
— Ministry of Health (@MOH_Kenya) June 26, 2023